1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Ulaya zaongoza uuzaji wa silaha

5 Desemba 2016

Makampuni ya silaha ya Marekani na Ulaya Magharibi yalihodhi katika biashara ya uuzaji silaha ulimwenguni mwaka 2015, wakati makampuni ya Urusi na Korea Kusini yakiwa pia yanaongezeka.

https://p.dw.com/p/2Tk1y
Barack Obama Waffengesetze in den USA
Picha: Reuters

Kwa mujibu wa taasisi inayochunguza masuala ya amani duniani yenye makao yake makuu mjini Stockholm, SIPRI, uuzaji wa vifaa vya kijeshi na huduma katika nchi 100 za juu duniani zenye silaha, zilikuwa na jumla ya dola bilion 370.7 ikishuka kidogo kwa asilimia 0.6 ukilinganisha na mwaka 2014.

Katika makampuni 39 ya kimarekani yaliyoorodheshwa kati ya makampuni makubwa 100 ya silaha, yanakamata mauzo kwa zaidi ya nusu ya silaha zilizouzwa ulimwenguni mwaka 2015

Mauzo katika makampuni ya kimarekani yalikuwa na jumla ya dola bilion 209.7, ikiwa chini kwa karibu asilimia 3, hali hiyo inaonya kupungua kwa kiwango cha matumizi nchini Marekani, kupanda kwa thamani ya sarafu ya dola pamoja na bidhaa  nyingine kama vile ndege za kivita.

Kampuni ya Lockheed Martin imefanya mauzo ya dola bilion 36.4 ikifuatiwa na kampuni hasimu ya Boeng kwa dola bilion 27.9, na ikifuatiwa pia na kampuni ya Uingereza BAE sytem kwa dola bilion 25.5

Makampuni yaliyoko Ulaya Magharibi yalishuhudia kuongezeka kwa mauzo mwaka 2015, na jumla ya uuzaji ulikuwa ni dola bilion 95.7 ililinganishwa na kushuka kulikoshuhudiwa mwaka 2014.

Makubaliano ya uuzaji silaha nje ya nchi wachangia ongezeko

Thailand Bangkok Nationaler Kindertag Soldat Kind MG
Mtoto akiwa ameshika silaha nchini ThailandPicha: picture-alliance/Pacific Press/V. Poti

Kuongezeka kwa kiasi kidogo cha asilimia 6.6 cha biashara ya silaha kwa makapuni ya Ulaya Magharibi kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na makubaliano ya uuzaji wa silaha nje ya nchi na makampuni ya kifaransa yaliyoko Misri na Qatar alisema Aude Fleurant kiongozi wa  SIPRI anayeshigulika na  mpango wa masuala ya matumizi ya silaha.

Pamoja na kuwa makampuni 10 makubwa  ya utengenezaji wa silaha yanapatikana nchini Marekani au Ulaya Magharibi yanatawala nusu ya mauzo ya silaha ulimwenguni mwaka 2015, SIPRI inasema kuwa mpango wa muda mrefu ambao unatazamiwa unaonyesha kuwa kuhodhi kwao kunadhoofika. Mwaka 2012 ushiriki wao ulikuwa karibu asilimia 60.

Makampuni ya Urusi na Korea Kusini yameongezeka pia katika uuzaji wa silaha, wakati ripoti hiyo ikikariri kuwa kuna uimara wa uzalishaji nchini India na Uturuki. Makapuni ya Urusi  yanasimamia chini ya asilimia 10 ya mauzo katika orodha hiyo, kampuni kubwa ya Urusi ilikuwa na mauzo ya dola bilion 6.9, katika nafasi ya jumla imeshika nafasi ya 13.

Manunuzi ya silaha ndani ya nchi pamoja na uuzaji wa silaha nje ya nchi umesaidia kuongeza mauzo ya silaha kwa karibu dola bilion 7.7 ya makampuni 7 ya Korea Kusini yaliyo katika orodha.

Kutokana na kutokuwepo kwa taarifa za kutosha makapuni ya China hayakuwekwa katika orodha, japo SIPRI inakadiria kuwa makapuni 9 ya kichina yangeweza kuingizwa katika orodha hiyo.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/DPA

Mhariri:Yusuf Saumu