Marekani Kuiregezea kamba Cuba kuliwadia zamani ? | Magazetini | DW | 15.04.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Marekani Kuiregezea kamba Cuba kuliwadia zamani ?

Na je, uamuzi wa kuruhusu sharia ni sawa huko Pakistan ?

default

( Barack Obama -na Cuba)

Moani ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo yamechambua mno uamuzi wa waziri wa kilimo kupiga marufuku uvunaji wa mahindi chapa "Mon 810" humu nchini yamnayopandishwa kwa njia za kim,aabara (genetic).Isitoshe, wahariri wameichambua siasa ya Rais Obama kuregeza vikwazo kwa Kuba;azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la UM dhidi ya Korea ya kaskazini na uamuzi wa Pakistan wa kuruhusu matumizi ya sharia katika mkoa wake wa kaskazini unaotawaliwa na wataliban.

Tukianza na gazeti la Neueste Nachrichten juu ya sera za rais Obama kuelekea Kuba,gauzeti laandika:

"Kusahihishwa kwa siasa ya marekani kuelekea Cuba anakofanya sasa Rais Barack Obama kuliwadia zamani na hakutokani kabisa na ubinadamu.Marufuku iliowekewa Cuba haikua na maana yoyote na ya kinafiki.Kwani, kuiadhibu Cuba kwa vikwazo kwa na wakati huo huo kujenga gereza la Guantanamo huko huko Cuba,ni mojawapo ya siasa za unafiki na za kutatanisha za utawala wa Bush. Lakini hata kwa Cuba,siasa mpya anayoifuata rais Obama inaibainishia saa ya kuutambua ukweli wa hali ya mambo imegonga.Hadi sasa Havana ikinyosha kidole cha hali mbaya za maisha nchini zikichangiwa na marufuku ya biashara iliowekewa Cuba.

Licha ya kuregezwa vikwazo,kumesalia bado vikwazo muhimu .Lakini hata vikwazo hivyo mwisho wake unaonekana sasa.Hadi vitakapoondoshwa vikwazo hivyo, itadhihirika iwapo rais Raul Castro ana uwezo wa kufanya mageuzi na ana hamu ya kufanya hivyo."

Likituchukua katika mvutano na Korea ya kaskazini, gazeti la Lausitzer Rundschau linalochapishwa Cottbus,laandika:

"Kamari unayocheza gengi linalotawala Korea ya kaskazini,isitiwe mno maanani.Muhimu sana ni kuzungumza na uongozi wa China kinaga naga,dhahiri-shahiri.Kwani, bila ya msaada wa China ,utawala wa Pyongyang ungejikuta matatani mno.

Ungeweza mnamo muda wa wiki chache tu kudhofishwa endapo viongozi wa Beijing wakiona yafaa kufanya hivyo.Bado lakini Beijing inamkumbatia mshirika wake pekee wa kinadharia .Kwamba China lakini haikulitia munda azimio la UM dhidi ya Korea ya Kaskazini,lazima kumeitia hofu Pyongyang."

Mannheimer Morgen, linauchambua uamuzi wa serikali ya Pakistan kuwaachia wataliban kutumia sharia katika jimbo lake la kaskazini la Swat-Tal.Laandika:

"Ni kuwanyoshea mkono wa amani ambao hauna hata thamani ya jina hilo.Rais Zadari wa Pakistan kwa kuridhia kutumika sharia katika eneo ambalo hadi sasa limekuwa kimya na la utulivu,hakufanya mema.na watalibani hawatacha shaka kuwa mapatano waliofunga nae ni ya kwanza tu.Kwani, haukupita muda, waakilishi wa watalibani wameshasema wanataka kueneza sharia hataka katika sehemu nyengine za Pakistan.na hivyo, hatua kwa hatua watalibani wanaimarisha madaraka na nguvu zao na sio tu nchini Pakistan.............."

Mwishoe, gazeti la Sudwest Presse linatuchambua uamuzi wa waziri wa kilimo wa Ujerumani kupiga marufuku jana mahindi yanayovunwa kwa njia za kimaabara-genetic.Laandika:

"Mafidhuli wanadai eti waziri wa kilimo huyo bibi Ilse Aigner amechukua hatua yake ya jana ya kupiga marufuku upandaji mahindi ya aina ya "Mon 810" nchini humu kutokana na kushinikizwa tu na mtangulizi wake katika wadhifa huu,waziri mkuu wa sasa wa Bavaria Bw.Horst Seehofer.Bw.seehoefer angependa pia kuitumia mada hii katika kampeni ya uchaguzi ujao...."

Mwandishi:Ramadhan Ali

Mhariri:M.Abdul-Rahman

 • Tarehe 15.04.2009
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HXDL
 • Tarehe 15.04.2009
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HXDL
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com