1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani haikubaliani na Korea ya Kaskazini

Sudi Mnette
16 Desemba 2019

Mjumbe maalumu wa Marekani katika mazungumzo yaliokwama ya Korea Kaskazini, Stephen Biegun amesema Marekani haikubaliani na muda wa mwisho wa mazungumzo ya nyuklia uliopangwa na Korea Kaskazini.

https://p.dw.com/p/3UsMB
Nordkorea | Neue Raketentests
Jaribio la kombora la masafa marefu la Korea KaskaziniPicha: Reuters/KCNA

Akizungungumza muda mfupi baada ya kuwasili nchini Korea Kusini alisema "Kwa hivyo, hapa leo, niwaeleze wenzetu Korea Kaskazini. Ni muda kwetu sote, kutimiza wajibu wetu. Tulifanye hili. Tuko hapa. Na unajua namna ya kutufikia. Tunataarifa za kina kwa uwezekekani madhubuti wa Korea Kaskazini kufanya matukio makubwa ya uchokozi katika siku zijazo. Kuendelea kwa vitendo hivyo itakuwa sio jambo la heri katika kufanikisha amani ya kudumu katika rasi ya Korea"

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani alikuwa mjini Korea Kusini kwa ziara ya kikazi ambapo ameitaka Korea Kaskazini kukukabli kuketi kwa ajili ya mazungumzo. Hata hivyo haijawa wazi kama Korea Kaskazini itakubali pendekezo hilo ili kuweza kudhibiti wigo wa tofauti ambao umezidi kupanuka katika mpango wa kuondosha matumzizi ya nyuklia ya Korea Kaskazini.

Msimamo wa Korea Kaskazini bado tata

Hivi karibuni maafisa waandamizi wa Korea Kaskazini wamesikika wakisema mazungumzo ya kuachana na matumizi ya nyuklia yamekwisafika ukomo na tayari yameanza kutoa vitisho vya matumizi ya nishati hiyo kwa kufanya majaribio ya kufyatua makombora ya masafa matrefu. Lakini kwa kauli hii ya sasa ya Marekani, Mwakilishi wa  mwakilisi maalumu wa Korea Kusini katika utafutaji wa amani na usalama katika Rasi ya Korea Lee Do-Hoon anasema "Kuhusiana na mazunguzo ya kusitisha matumizi ya nyuklia, Biegan amesisitia hakutakuwa na mabadiliko kwa Marekani. Mzozo utapaswa kutatuliwa kwa mazungumzo na diplomasia. Na amehakikisha masuala yote yenye maslahi kwa Korea Kaskazini yatazingatiwa endapo mazungumzo yataanza."

Hofu ya kuongezeka kwa vitendo vya uchokozi kwa Korea Kaskazini iliongezeka baada ya taifa hilo kusema Jumamosi iliyopita limefanikiwa kile ilichokitaja jaribio muhimu, ambalo linaweza kuongezea uwezo katika kuzuia makombora ya nyuklia. Wataalamu wanasema Korea Kaskazini inaweza kurusha satellite yenye wa kubeba roketi au kombora la masafa marefu, endapo Marekani itashindwa kufikia muda wa mwisho wa mazungumzo, ambao ulipangwa kuhitimishwa mwishoni mwa mwaka huu.

Jaribio hilo la Ijumaa ni la pili kufanyika katika juma moja, katika eneo la kiwanda cha roketi, ambalo Korea Kaskazini ilifanya jaribio lingine la ambalo Umoja wa Mataifa ilisema jaribio lenye kuonekana kama la kombora la masafa marefu la teknolojia ya kisasa.