1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kudhibiti wahamiaji waandaliwa

10 Juni 2022

Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wenzake wa Amerika Kaskazini na Amerika Kusini wanatarajiwa kutangaza mpango unaolenga kudhibiti uhamiaji haramu na kushughulikia idadi kubwa ya wahamiaji.

https://p.dw.com/p/4CXZ6
Americas Gipfel Biden Bolsonaro
Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wenzake wa Amerika Kaskazini na Amerika Kusini wanatarajiwa kutangaza mpango unaolenga kudhibiti Uhamiaji wazuwiwa kwa muda Marekaniharamu na kushughulikia idadi kubwa ya wahamiaji. Mpango huo uliopewa jina la Tamko la Los Angels, na kuelezewa na Biden kuwa wa kihistoria, unanuiwa kuzipa marupurupu nchi zinazoichukua idadi kubwa ya wahamiaji, na kugawa jukumu la changamoto hiyo ya uhamiaji kote katika kanda hiyo.  soma 

Mpango huo wa uhamiaji umefikiwa katika mkutano wa kikanda ulioandaliwa na Biden mjini Los Angeles ambao ulitengenezwa kwa ajili ya kuthibitisha uongozi wa Marekani na kukabiliana na kuongezeka kwa ushawishi wa kiuchumi wa China katika kanda hiyo.

soma Biden ayafuta maagizo ya Trump juu ya mazingira na uhamiaji

Mkutano huo wa kilele wa mataifa ya Amerika ulikumbwa na mzozo hata kabla haujaanza, kwani Biden alikataa kuwaalika viongozi wa mrengo wa kushoto wa Cuba, Nicaragua na Venezuela kwa misingi kwamba wao ni wababe.

Mexico na mataifa kadhaa ya Amerika ya Kati ambayo ni wahusika wakuu, pamoja na Haiti, walikataa kutuma viongozi wao kwenye mkutano huo wa Kilele wa wiki moja wa uliofanyika mjini Los Angeles.

soma EU kupendekeza mageuzi ya mfumo wa uhamiaji, wakimbizi

Suala zito kwa siasa za Marekani

Amerika-Gipfel in Los Angeles Biden
Rais BidenPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Uhamiaji umekuwa suala zito la kisiasa huko Washington kwani umaskini, ghasia na majanga ya kitaifa yamesababisha kuongezeka kwa Waamerika ya Kati na Wahaiti wanaotaka kuingia Marekani.

Wabunge wa chama cha Republican cha rais wa zamani Donald Trump wameshikilia suala hilo,  akiwashutumu wahamiaji wengi na kumshutumu Biden kwa kushindwa kuchukua hatua ipasavyo.

Uhamiaji umezidi ulimwenguni kote, huku mamilioni ya Wavenezuela pia wakikimbia uchumi unaoporomoka.

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alisusia mkutano huo kulalamikia kutengwa, na viongozi walikosoa uamuzi huo kwa Biden katika kikao cha mawasilisho jana Alhamisi.

Waziri mkuu wa taifa dogo la Amerika ya Kati, Belize, John Briceno, alimkosoa Biden moja kwa moja na kumwambia kwamba vikwazo vya muda mrefu vya Marekani kwa Cuba ya kikomunisti ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Biden, ambaye alipiga makofi kwa heshima na kusalimiana na kila kiongozi, alirejea jukwaani kusema kwamba ajenda yake iko sawa.

Hata hivyo utawala wa Biden umejitenga na matangazo ya makubwa ya kifedha na badala yake umezingatia matamko mapana na kuahidi kuyafanyia kazi maalum baadaye.

Utawala uliahidi wakati wa mkutano wa kilele wa wiki nzima kufanya kazi ya kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wa afya 500,000 katika Amerika na kuzindua ufadhili wa dola bilioni 1.9 katika sekta ya kibinafsi kwa Amerika ya Kati ili kuunda nafasi za kazi na kumaliza baadhi ya sababu za uhamaji.

 

AP/ AFP