Marehemu rais Umaru YarÁdua wa Nigeria azikwa leo | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.05.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Marehemu rais Umaru YarÁdua wa Nigeria azikwa leo

Goodluck Jonathan hii leo ameapishwa kiongozi mpya wa Nigeria, saa chache baada ya Rais Umaru YarÀdua aliekuwa na miaka 58 kufariki jana Jumatano baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Bildausschnitt von Jonathan Goodluck. French Prime Minister Francois Fillon, left, stands with Nigerian d Vice President Goodluck Jonathan as he meets for talks with leaders of Africa's most populous nation, at the Presidential Villa in Abuja, Nigeria Friday, May 22, 2009. Fillon later told reporters that France was Nigeria's second-largest investor after the United States, and he praised Nigeria for contributing to peacekeeping missions across Africa. (AP Photo/Abayomi Adeshida)

Rais mpya wa Nigeria, Jonathan Goodluck.

Goodluck Jonathan mwenye umri wa miaka 52 leo ameapishwa rais mpya wa Nigeria, nchi iliyo na wakaazi wengi kabisa barani Afrika na inayokabiliwa na mivutano ya kidini na kisiasa. Baada ya kupokea madaraka yake mapya, Jonathan aliahidi kufanya marekebisho katika utaratibu wa uchaguzi ujao na kupiga vita ulaji rushwa na akaongezea:

"Hata jitahada za kuendeleza amani na maendeleo katika Niger Delta na juhudi za kulinda maisha na milki kote nchini ni kipaumbele."

Jonathan tayari alikuwa akiongoza shughuli za serikali kama rais wa mpito na hakuna mabadiliko makubwa yanayotazamiwa katika sera za serikali. Kwani YarÁdua alitoweka kwenye jukwaa la kisiasa tangu Novemba mwaka jana alipokwenda Saudi Arabia kwa matibabu ya moyo. Alirejea Nigeria mwezi wa Februari lakini hali yake ya afya haikumruhusu kufanya kazi na hakuonekana tena hadharani.

Jonathan alieshika madaraka miezi mitatu iliyopita, ameshafanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na amewateua washauri wake tangu wakati huo. Sasa atamteua makamu wa rais na serikali hiyo inatazamiwa kubakia madarakani hadi muhula wa rais uliobaki utakapomalizika mwakani na uchaguzi kuitishwa mwezi wa Aprili. Haijulikani iwapo Jonathan anaetokea Niger Delta atagombea urais katika uchaguzi ujao. Kwani katika chama tawala, kuna makubaliano yasio ya kimaandishi, kuwa wadhifa huo unakwenda kwa zamu, kati ya kaskazini na kusini. Na muhula ujao wa miaka minne ni zamu ya Waislamu wa kaskazini. Suala muhimu ni nani atakaekuwa makamu mpya wa rais. Huyo huenda akatokea kaskazini na ndie atakaegombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2011.

Umaru Musa Yar'Adua (* 1951 in Katsina) ist ein nigerianischer Politiker und seit 2007 Staatspräsident Nigerias. Umaru Yar'Adua, waits to make his acceptance speech after he was declared winner at the People's Democratic Party (PDP) primary elections in Abuja, Nigeria, Sunday, Dec. 17, 2006. Nigeria's ruling party on Sunday chose a Muslim from the north as its candidate in next year's presidential elections. Governor Umaru Yar'Adua of Katsina, had won 3,024 votes _ easily beating his closest rival, who received only 372 votes. (AP Photo/George Osodi)

Marehemu Rais Umaru YarÁdua wa Nigeria.

Marehemu YarÁdua alieahidi kuheshimu utawala wa kisheria aliposhika madaraka, alitoa matumaini kwa wananchi wengi, baada ya kumalizika utawala wa miaka minane wa rais wa zamani Olusegun Obasanjo, aliekuwa kiongozi wa kijeshi hapo awali na aliependa kupuuza amri za mahakama na kanuni zake. YarÁdua alishinda uchaguzi uliofanywa Aprili mwaka 2007 na kwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo kupata uhuru wake katika mwaka 1960, serikali za kiraia zilipokezana madaraka.

Maiti ya marehemu YarÁdua imepelekwa mji wa Katsina alikozaliwa na anazikwa huko hii leo. Maelfu ya watu wamekusanyika uwanja wa ndege na wengine wamepangana barabarani. Mkaazi mmoja wa Katsina amesema,kifo cha rais YarÁdua ni hasara kubwa kwa demokrasia, kwa Nigeria na bara zima la Afrika.

Mwandishi: P.Martin/RTRE/AFPE

Mhariri: M.Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com