1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marais 3 wa ECOWAS kwenda Abidjan

26 Desemba 2010

Marais watatu wa mataifa ya Afrika Magharibi wanatarajiwa kwenda nchini Corte d´Voire keshokutwa Jumanne kumtaka kiongozi wa nchi hiyo Laurent Gbagbo aondoke madarakani kwa hiyari yake au zitumike nguvu.

https://p.dw.com/p/zpxH
Kiongozi wa Ivory Coast Laurent GbagboPicha: AP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Benin, Jean Marie Ehouzou, amesema marais hao kutoka Benin, Siera Leone na Cape Verde, watamwambia bwana Gbagbo aondoke haraka madarakani na kumkabidhi nchi Alassane Ouattara, au vinginevyo ataondolewa kwa nguvu za kijeshi.

Gbagbo amekataa wito huo na kusema kuwa si tishio la haki.Kwa upande mwengine Umoja wa Mataifa umesema kuwa kiasi cha wakimbizi 14,000 wameikimbia nchi hiyo na kuingia katika nchi jirani ya Liberia, wakihofu kuibuka tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tayari kiasi cha watu 200 wamekwishauawa, tokea kuibuka kwa vurugu kutokana na uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Mohamed Dahman