1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPUTO : Ghala la silaha laripuka

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7I1

Madarzeni ya wakaazi wamehamishwa leo hii baada ya ghala la silaha kuripuka huko Inhamizua karibu na mji wa pili kwa ukubwa nchini Msumbiji wa Beira.

Mripuko huo umesababishwa na wakulima waliokuwa wakichoma mashina ya nyasi karibu na ghala hilo.Ingawa hakuna maafa au majeruhi nyumba nyingi zimeharibiwa na mripuko huo.

Miezi saba iliopita zaidi ya watu 105 waliuwawa katika tukio kama hilo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo.

Serikali inadai tokea kutokea kwa tukio hilo imeteketeza tani 400 za silaha kongwe zisizotumika kupunguza hatari ya miripuko.