1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko yaua zaidi ya watu 23 Burundi

Lilian Mtono
5 Desemba 2019

Zaidi ya watu 23 wameripotiwa kufariki kutokana na maporomoko ya mlima yaliyoangukia nyumba za wakaazi katika kijiji cha Nyabundu tarafa ya mugina mkoani Cibitoke magharibi mwa Burundi.

https://p.dw.com/p/3UGHC
Brasilien Bodenprofil am Amazonas Lateritboden unter tropischem Regenwald
Picha: Imago Images/blickwinkel

Taarifa kutoka eneo hilo la Nyabundu tarafa ya Mugina katika mkoa wa Cibitoke zinasema mvua nyingi zilizonyesha usiku wa jana kuamkia leo zimepelekea mlima ulio katika eneo hilo kukabiliwa na mmomonyoko wa ardhi na maporomoko ya tope zilizosababisha mfuriko katika majumba yaliyo katika eneo hilo.

Leonard Habonimana raia mkaazi wa mkoani huo wa cibitoke ameiambia DW kwa njia ya simu kuwa mvua ni nyingi mno katika eneo. Na kwamba hadi saa mbili asubuhi maiti za watu 6 zilikuwa tayari zimeondolewa chini ya udongo ambao uliifunika kwenye eneo la Mugina. Raia huyo amesema tayari milima mitatu imemomonyoka katika eneo hilo la Mugina.

Südsudan Überschwemmungen Hütten
Mvua zimetajwa kuleta maafa makubwa nchini Burundi, ikiwa ni pamoja na mafurikoPicha: Getty Images/AFP/P. Louis

Saa moja kabla ya kuingia hewani mkuu wa tarafa ya Mugina amebaini kuwa tayari miili ya watu 23 imeondolewa eneo hilo na kwamba shuhuli za uokozi bado zinaendelea.

Hata hivyo eneo kuliko tokea mafuriko hayo na maporomoko ya ardhi limetajwa kuwa umbali wa kilometa kama 5 hivi na makao makuu ya tarafa ya Mugina.

Mvua nyingi zimekuwa zikinyesha mnamo siku za nyuma nchini humu na kusababisha mafuriko makubwa. Mwezi Oktoba watu wengine wa 6 walipoteza maisha katika mtaa wa Carama kaskazini mwa jiji la Bujumbura.

Burundi imekuwa ikikabiliwa na athari za tabia nchi ambapo jua kali limekuwa likiharibu mimea mashambani na kusababisha njaa hususan katika mkoa ya kaskazini mwa nchi pamoja na mvua zilizosababisha mafuriko na maafa.