Mapigano yazuka upya Mashariki mwa Kongo | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.09.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mapigano yazuka upya Mashariki mwa Kongo

Nchini Kongo mapigano yanaripotiwa kuzuka upya baina ya waasi wanaoongozwa na Jenerali muasi Laurent Nkunda na wanajeshi wa serikali ya Kongo kwenye eneo Tamugenga mkoani Kivu ya Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Mapigano dhidi ya waasi wa Laurent Nkunda Mashariki mwa Kongo yazuka upya

Mapigano dhidi ya waasi wa Laurent Nkunda Mashariki mwa Kongo yazuka upya

Mapigano hayo yalitokea kufuatia maandamano ya raia wa Rutchuru hapo jana ambapo kifaru kimoja cha jeshi kilichomwa na wanajeshi wawili wa Umoja wa Mataifa kujeruhiwa.Itakumbukwa kuwa makubaliano ya amani yalitiwa saini mwezi Januari mwaka huu japo mapigano bado yanazuka mara kwa mara.

Kutoka Goma mwandishi wetu John Kanyunyu ametuandalia taarifa ifuatayo.


Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com