Mapigano ya kikabila nchini Kenya | Matukio ya Afrika | DW | 29.08.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Mapigano ya kikabila nchini Kenya

Hali bado ni ya taharuki katika kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya baada ya watu 20 kuuwawa kutokana na mapigano ya kikabila yaliyotokea jana mchana.

Bado ukabila ni tatizo nchini Kenya

Bado ukabila ni tatizo nchini Kenya

Mapigano hayo kati ya kabila la Borana, Gabbra na Burji yanasemekana kusababishwa na mzozano wa ardhi na pia kuchochewa kisiasa.

Hata hivyo polisi wamepelekwa katika eneo hilo la Marsabit kuimarisha usalama na kwa sasa pole pole hali inasemekana kuwa ya kawaida japo hofu kubwa bado imetanda miongoni mwa wakaazi kufuatia kuzuka tena kwa mapigano.

Muda mfupi uliopita Amina Abubakar amezungumza na Sheikh Adan Wachu ambaye yuko katika kamati ya kutafuta amani katika eneo hilo, kwanza anaelezea hali halisi ilivyo katika eneo hilo kwa sasa. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada