1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano makali yaendelea Sudan

Saleh Mwanamilongo
5 Mei 2023

Licha ya matamko mengi ya kusitisha mapigano, pande hasimu bado zinapigania udhibiti wa maeneo katika mji mkuu Khartoum, kabla ya mazungumzo yaliyopendekezwa.

https://p.dw.com/p/4QwYb
Juhudi za kidiplomasia bado kumalizisha mapigano Sudan
Juhudi za kidiplomasia bado kumalizisha mapigano Sudan Picha: AFP/Getty Images

Hadi sasa majenerali wawili wanaohasimiana wameonyesha nia ndogo ya kufanya mazungumzo baada ya zaidi ya wiki mbili za mapigano.

Katika vita vikali, jeshi la Sudan jana Alhamisi lilitaka kuwaondoa wapiganaji wa kikosi cha usaidizi wa haraka,RSF, kutoka maeneo wanakodhibiti katikati mwa Khartoum.

Avril Haines, mkuu wa shirika la ujasusi wa taifa nchini Marekani ameiambia kamati ya usalama ya Seneti ya nchi hiyo kuwa kila upande unaozozana nchini Sudan unategemea ushindi wa kijeshi na pande hizo mbili hazina motisha ya kukaa kwenye meza ya mazungumzo. Tayari ikulu ya Marekani imetishia kuwawekea vikwazo wale wanaoyumbisha usalama wa Sudan.

Machafuko hayo ya Sudan yamesababisha vifo vya mamia ya raia , huku maelfu wengine wakikimbilia  nchi jirani.

''Vurugu hizo laima zikome''

Mashirika ya misaada yajitahidi kutioa misaa kwa wakimbizi
Mashirika ya misaada yajitahidi kutioa misaa kwa wakimbiziPicha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Catherine Russell, mkurungezi wa Shirika la Umoja wa Matifa la kuhudumia watoto UNICEF amesema katika taarifa yake kwamba hali nchini Sudan inaelekea kwenye janga na watoto wanazidi kuathirika na mzozo huo. Russell amesema kwa ajili ya watoto wa Sudan vurugu hizo lazima zikome.

Mkuu huyo wa UNICEF amesema mashambulizi yamepunguza uwezo wa shirika hilo kutoa misaada kwa watoto kote nchini. UNICEF imesema imepokea ripoti ya watoto 190 waliouawa na wengine 1,700 kujeruhiwa nchini Sudan tangu mzozo kuanza Aprili 15. Hata hivyo nivigumu kufahamu idadi halisi kutokana na ukubwa wa vurugu,limesema shirika hilo.

Kwa upande wake shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR,limetoa mwito kwa serikali za nchi jirani ya Sudan kuwapokea wakimbizi na kutowaruhusu kurejea makwao. Kauli hiyo inafuatia taarifa kwamba kulikuwa na msongamano wa watu kwenye mpaka wa Sudan na Misri.

Mito ya misaada ya kibinadamu

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mzozo nchini Sudan umewalazimu takriban watu 100,000 kukimbilia nchi jirani, na kuzuia utoaji wa misaada katika nchi hiyo ambayo karibu theluthi moja ya watu tayari walitegemea msaada wa kibinadamu.

Huku hayo yakiendelea, taarifa kutoka Geneva zimesema shirika la mpango wa chakula ulimwenguni, WFP limeripoti upotevu wa bidhaa za vyakula zenye thamani ya kati ya dola milioni 13 na 14 zilizopaswa kupelekwa Sudan, tangu kulipozuka mapigano hayo.