1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano makali Syria

13 Machi 2013

Waasi wa Syria wana miazi 2 tu ya kuiteka barabara kuu itokayo mjini Damascus kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo, licha ya kukabiliwa na mapigano makali kutoka kwa vikosi vya utawala wa Bashar Al-Assad

https://p.dw.com/p/17vtl
Free Syrian Army fighters eat atop an armoured personnel carrier, that belonged to forces loyal to president Bashar al Assad, at the police academy in Aleppo, after capturing it March 4, 2013. On Sunday rebels said they captured a police academy on the outskirt of Aleppo, after days of fighting in which rebels killed 150 soldiers, while sustaining heavy casualties. REUTERS/Mahmoud Hassano (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Waasi wa SyriaPicha: Reuters

MAPIGANO makali yametokea katika mji wa Homs nchini Syria katika ya  waasi na vikosi vya utawala wa Rais Bashar Al-Assad na kukata mawasiliano ya  barabara kuu inayounganisha mjini wa Damascus na uwanja wa ndege wa kimataiafa wa nchi hiyo.

Hayo yamesemwa na  waangalizi wa shirika  la kutetea haki za binadm  nchini Syria wakiongea na shirika la habari la AFP. Mapigano hayo yanakujawiki moja baadaya utawala wa Rais Bashar Al-Assad kupeleka vikosi vyake  ili kuwaondoa waasi wanaodhibiti mji wa Khaldiyeh karibu na mji  mkuu wa Syria Damascus.

Kauli ya waangalizi katika mapigano

''Waasi na vikosi vya utawala wa Rais Bashar Al-Assad wamekuwa katika  mapambano makali katika eneo la Baba Amr. Mapigano hayo yalizidi hasa katika  barabara ya   Brazil street, na vikosi vya utawala wa Syria vinadaiwa kutumia mabom na makombora ambayo yamehharibu vibaya mji wa Khaldiyeh''wamsema waangalizi wa haki za binadam.

Rebels fighters prepare to fire a portable canon against an adjacent Syrian government-held building during fighting on February 27, 2013 in the Hawiqah neighbourhood of the eastern Syrian town of Deir Ezzor. Syria's opposition and foreign powers hold crucial talks in Rome with Washington suggesting it is ready to boost support to rebels in their struggle against President Bashar al-Assad. AFP PHOTO/ZAC BAILLIE (Photo credit should read ZAC BAILLIE/AFP/Getty Images)
Waasi wa SyriaPicha: ZAC BAILLIE/AFP/Getty Images

Mapigano mapya pia yametokea katika  jana katika  eneo la  Baba Amr, ambalo linatajwa kuwa ni eno muhimu na jirani ambalo limekuwa ngome ya utawala wa Rais  Bashar al-Assad.

Mapigano katika mji wa Babr Amr

Mapema  wiki hii  waasi wa Syria walipanga kufanya mashambulizi makubwa ili kurudisha mji wa  Babr Amr, ambao ulitokea mapigana ya silaha  katika ya waasi na vikosi vya utawala wa Bashari Al -Assad

Mapigano hayo yanafanyika katika  eneo hilo, kutokana na barabara hiyo kuwa muhimu na ndio njia kuu  ya utawala wa Syria kuondoka nje  ya nchi, na kuwa karibu zaidi na mji mkuu wa Syria Damascus.

Jana mapambano makubwa yameshuhudiwa Mashariki ya mji wa Jobar, ambapo waasi walikuwa wanadhibiti pembeni ya mji huo. Ni miaka miwili sasa Syria  ikiwa katika  machafuko ya kisisa ambayo yamepelekea zaidi ya watu  70,000   kufariki dunia  na maelfu ya wengine  kuishi wakiwa wakimbizi katika maeneo ya chi jirani ya Syria.

Mwandishi:  Hashim Gulana/ AFP & Reuters
Mhariri:  Moahammed Abdul-Rahman