1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini.

Mtullya, Abdu Said18 Juni 2008

Magazeti ya Ujerumani yatoa maoni juu ya hotuba ya rais Horst Köhler.

https://p.dw.com/p/EMDY
Rais Horst Köhler wa Ujerumani wakati akitoa hotuba mjini Berlin.Picha: picture-alliance/dpa

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amewataka wajerumani wasonge mbele na mageuzi yaliyoleta ustawi wa uchumi na nafasi za ajira mnamo miaka mitatu iliyopita.

Rais Köhler amesema hayo katika hotuba ya kila mwaka anayotoa kwa taifa. Katika maoni yao magazeti ya Ujerumani leo yanazungumzia juu ya hotuba hiyo.

Gazeti la Aachener linasema ,katika hotuba yake rais Köhler ametahadharisha ,amehimiza , amepongeza na amekosoa.Gazeti linatilia maanani kwamba rais huyo ameikosoa sheria ya kodi ambayo ni ya kutatanisha. Pia ameukosoa mfumo wa kodi.Amesema mfumo huo ni mzigo mkubwa kwa watu fulani. Gazeti linasema hayo yote ni sawa, lakini hakuna mpango maalaum.Kinachotakiwa ni umakinifu ili kutayarisha mpango huo.

Gazeti la Westfalenpost linampongeza rais wa Ujerumani kwa hotuba yake ya mjini Berlin lakini linasema , kuhusu nyanja fulani angeliweza kupunguza rangi ya waridi.

Na badala yake angeliweza kusisitiza juu ya masuala ya uhaba wa raslimali, mabadiliko ya hali ya hewa na mgogoro wa fedha duniani. Lakini gazeti linasema, katika upande mwingine masuala hayo yanafahamika.

Mhariri anatilia maanani kuwa rais Köhler kwa mara nyingine amezungumzia juu ya masuala ya umasikini na elimu ; lakini swali ni jee wajerumani wanapaswa kusikia juu ya masuala hayo kutoka kwa rais wao?

Badala ya kuzungumzia juu ya demokrasia,Ujerumani na juu ya dunia nzima katika hotuba moja, rais Köhler angelijaribu kutuama katika suala moja tu. Hayo anasema mhariri wa gazeti la Westdeutche Allgemeine.

Kwa mfano ingekuwa bora kwa rais huyo kuzungumzia juu ya demokrasia tu na kufafanua. Hatahivyo gazeti linatilia maanani kauli ya rais huyo juu ya kuimarisha demokrasia nchini Ujerumani kwa kuwapa wananchi ushawishi mkubwa zaidi katika kuamua juu ya orodha za wajumbe wastahiki.

Gazeti linakubaliana na pendekezo hilo, lakini ushauri wa rais huyo juu ya kurefusha muhula wa bunge hadi kufikia miaka mitano, na juu ya kufanyika uchaguzi wa majimbo na serikali za mitaa katika siku moja-ushauri huo utapunguza demokrasia nchini Ujerumani.

Gazeti la Saarbrücker linasema hotuba ya rais Köhler haikupokelewa kwa mikono miwili na wanasiasa wote wa Ujerumani.Mhariri wa gazeti hilo anatamka kuwa baadhi ya wanasiasa hao wanamwona rais Köhler kuwa ni mtu anaejifanya mjuzi wa kila kitu.Lakini mhariri huyo anawaambia wanasiasa hao, wajaribu kuzingatia aliyosema rais huyo juu ya demokrasia na juu ya kusonga mbele na sera za mageuzi.