Maoni ya wahariri. | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 15.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Maoni ya wahariri.

Katika maoni yao wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanatoa maoni juu ya juhudi za rais G .W Bush katika mashariki ya kati na juu Da Lai Lama.

Rais wa Marekani G.W.Bush na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert.

Rais wa Marekani G.W.Bush na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert.

Katika maoni yao leo wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia juu ya juhudi za rais George W. Bush katika mashariki ya kati na juu ya uhusiano baina ya serikali ya Ujerumani na Da Lai Lama.

Gazeti la Badische Zeitung linasema,katika macho ya wapalestina rais Bush amepoteza uadilifu katika kusuluhisha mashariki ya kati.

Gazeti hilo linauliza jee rais G .W.Bush alikuwa wapi siku zote mpaka sasa ajaribu kuleta suluhisho la haraka katika eneo hilo?

Kwa hiyo wapalestina hawamwoni rais huyo kuwa ni msuluhishi wa kweli.

Magazeti leo pia yametupia macho uhusiano baina ya serikali ya Ujerumani na kingozi wa kidini wa watu wa Tibet Da Lai Lama.

Gazeti la Nordbayerishe Kurie linakumbusha kwamba Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikutana na kiongozi huyo wa watibet. Merkel alilaumiwa na makamu mwenyekiti wa chama cha SPD kwa sababu ya mkutano huo.

Lakini sasa makamu mwenyekiti huyo,Steinmeier ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani anamtuma waziri mwenzake kwenda kukutana na Da Lai Lama.

Juu ya mkakati huo wa Steinmeier mhariri wa gazeti la Nordbayerische Kurie anasema ,mkakati huo asilani hautabadili ukweli kwamba bwana Steinmeier ndiye sasa anaeonekana kuwa mtu asiyejali sana haki za binadamu katika jimbo la China la Tibet na kwamba anaweka siasa mbele ili kuepusha mgongano na China nchi yenye manufa makubwa ya kibiashara kwa Ujerumani.


 • Tarehe 15.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E0HT
 • Tarehe 15.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E0HT
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com