Maoni ya wahariri | Magazetini | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri

Mkasa wa kijana huyo alierukwa akili ulitokea kwenye shule moja katika mji wa Emsdetten katika jimbo la Northrhein Westfalia kaskazini mwa Ujerumani . Alienda kwenye shule hiyo ambapo alisoma hapo awali na kuanza kuwashambulia watu kwa bunduki na mabomu na kuwajeruhi 37. Na baadae alijiua. Wahariri wa magazeti leo wanatoa maoni yao juu ya mkasa uliotokea kwenye shule ambapo kijana alierukwa akili aliwajeruhi watu 37 na kujiua baadae. Wahariri hao pia wanazungumzia juu ya kugunduliwa njama za magaidi za kutaka kuishambulia ndege ya abiria.

Juu ya tukio hilo la mhariri wa gazeti la OSTSEE-ZEITUNG la mjini Rostock mashariki mwa Ujerumani anasema kuwa jamii siku nyingi ilisalimu amri mbele ya watu kama hao wanaotenda ukatili. Mipaka ya maadili imeanguka na miiko yote inavunjwa mtindo mmoja.

Mhariri huyo anatalia maanani kwamba watu wanaorukwa akili kama kijana huyo wanaiga yanayooneshwa katika kompyuta,televisheni ama hata katika magazeti. Gazeti linasema , kutokana na kutokuwapo moyo wa kuwajibika miongoni mwa jamii matumizi ya vitu hivyo hayana mpaka

Naye mhariri wa gazeti la MITTELBAYERISCHE kutoka mji wa Regensburg ,katika maoni yake anatoa mwito kwa jamii, iwe macho. Anasema watu wanapasawa pia kuuliza maswali, hata yale yanayokera.. kwa mfano kwa nini kijana huyo aliekuwa anakabiliwa na kesi kutokana na kumiliki silaha kinyume cha sheria aliweza kuwa na mlundiko wa silaha bila ya mtu yeyote kujua?

Mhariri wa gazeti la EXPRESS kutoka mji wa Cologne anatoa mwito juu ya malezi bora kwa watoto wa shule wenye matatizo.

Mhariri huyo anatao mfano wa watoto ambao mara nyingi ni wapweke na wakimya. Gazeti linasema ukimya kama huo unaweza kuwa unaficha -chuki ya dunia nzima na hata kufikia kiwango cha kijana kujichukia mwenyewe. Gazeti linashauri haja ya kuwashughulikia vijana na watoto kama hao. Ni vizuri kuzumgumza nao badala ya kujenga utepetevu juu yao na kuwaacha wajifungie ndani wakitazama michezo ya kompyuta juu ya ukatili.

Ikiwa hayo yote yanafahamika kwa nini basi hatua hazichukuliwi , anauliza mhariri wa gazeti la BADISCHE . Au idadi ya watu wanaorukwa akili kama kijana huyo bado haijatosha ?

Wahariri wa magazeti leo pia wanazungumzia juu ya kugunduliwa njama za magaidi waliokusudia kushambulia ndege za abiria. Kutokana na uhodari wa polisi maafa yaliepushwa. Juu ya hayo gazeti la NORDBAYERISCHE KURIER linashauri haja ya kuwapo sera ya kuchunguza sababu za ugaidi na kuzikabili. Mhariri wa gazeti hilo anakumbusha kwamba katika mashambulio ya terehe 11 mwezi septemba nchini Marekani ndege za abiria ziligeuzwa mabomu

Na tokea wakati huo watu wana hofu.Na nchini Ujerumani hofu hiyo imeongezeka. Mhariri anasema safari hii imewezekana kugundua njama hizo na kuepusha maafa lakini, anaeleza mhariri huyo, magaidi asilani hawataacha kujaribu tena.

Lakini jambo muhimu sana anasisitiza mhariri huyo ni kukabiliana na mambo yanayosababisha ugaidi. Anasema hisia za kigaidi zinasababishwa pia na sera za kutumia mabavu zinazotekelezwa na nchi fulani .

Inapasa kuitafakari sera hiyo vizuri sana anasema mhariri huyo.