1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa Wakurdi unahitaji mazungumzo

Admin.WagnerD31 Desemba 2015

Wahariri wa magazeti wanasema kukombolewa kwa mji wa Ramadi, nchini Irak, ni hatua mojawapo tu katika juhudi za kupambana na magaidi wanaoitwa dola la Kiislamu.

https://p.dw.com/p/1HW48
Mji wa Ramadi wakombolewa
Mji wa Ramadi wakombolewaPicha: Getty Images/AFP/A. Al-Rubaye

Gazeti la "Berliner Morgenpost" juu ya dalili za kuanza kusambaratika kwa magaidi wanaoitwa dola la kiislamu .Mhariri wa gazeti hilo anazungumzia juu ya kukombolewa kwa mji wa Ramadi nchini Irak. Anasema kukombolewa kwa mji huo ni hatua mojawapo tu katika juhudi za kuwashinda magaidi.


Mhariri wa gazeti la "Süddeutsche" anatilia maanani kwamba magaidi wanatimuliwa nchini Irak na Syria, lakini katika nchi nyingine kama vile Libya,Tunisia na Misri,watu hao bado wana nguvu. Ndiyo sababu mhariri huyo anashauri umuhimu wa kuweka mikakati ya kisiasa, katika juhudi za kuwashinda magaidi.

Al-Bagdadi abezwa

Gazeti la "Wetz-larer Neue Zeitung" linasema ujumbe wa kiongozi wa magaidi al-Bagdadi unabezwa na Waislamu.Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba kiongozi wa "dola la Kiislamu, Abu Bakr al- Bagdadi amewataka Waislamu wote wajiunge na vita vya jihadi dhidi ya anaowaita makafiri !

Al-Bagdadi hakupiga vizuri hesabu zake. Matokeo yake ni kwamba amejigeuza kichekesho mbele ya Waislamu wa dhati. Waislamu hao wanamdhihaki kwenye mitandao ya kijamii. Mhariri anasema ujumbe unaostahili kutolewa ni mmoja tu, kwamba katika juhudi za kupambana na hatari ya magaidi binadamu wote wapendao amani wamesimama pamoja.


Iran imeanza kuyatekeleza makubaliano iliyofikia na mataifa makubwa juu ya mpango wake wa kinyuklia. Mapema wiki hii iliyapeleka madini yake ya uran, kurutubishwa nchini Urusi, kwa madhumuni ya amani. Gazeti la "Frankfurter Rundschau" linasema Iran imeitimiza dhima yake juu ya makubaliano na mataifa makubwa sita.

Rais wa Iran Hassan Rohani
Rais wa Iran Hassan RohaniPicha: picture-alliance/Geisler-Fotopress

Kwa kiwango kikubwa inaonekana kana kwamba nchi hiyo haitaunda silaha za nuklia. Na ikiwa lengo hilo litafikiwa migogoro itapungua katika Mashariki ya Kati. Hata hivyo shabaha hiyo haitajileta yenyewe.

Mdahalo utautatua mgogoro wa Wakurdi

Mhariri wa "Südeutsche anasema mgogoro wa Wakurdi nchini Uturuki unahitaji mdahalo. Anakumbusha kwamba tangu mwaka wa 1984 watu wapatao 40,000 wameshakufa kutokana na mgogoro huo.Mhariri anahoji kwamba huo ni ushahidi thabiti kwa Uturuki, kwamba, tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwa njia ya mabavu. Hata hivyo serikali ya Uturuki inatumia nguvu, kwa kisingizio cha kuulinda umoja wa kitaifa ingawa dunia inajua fika kwamba Uturuki imegawika

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Iddi Ssessanga