1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini.

Aboubakary Jumaa Liongo17 Desemba 2008

Katika maoni yao wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya kuzinduliwa kwa chama kipya cha kisiasa nchini Afrika Kusini.Hatua hiyo ni muhimu kwa demokrasia nchini humo

https://p.dw.com/p/GHv2
Kiongozi wa Chama kipya cha kisiasa nchini Afrika Kusini cha COPE Mosiuoa Lekota.Picha: AP

Pia wanazungumzia  juu ya  malengo  ya rais   mteule  wa  Marekani, Barack Obama.

Na magazeti ya Volksstimme na Neue Osnabrücker  yanatathmini yaliyotekelezwa na   rais Sarkozy  wa Ufaransa  katika  kipindi cha miezi sita iliyopita  ambapo aliuongoza Umoja  wa Ulaya.

Juu ya Afrika  ya  Kusini  gazeti la Berliner  Zeitung linasema  kuzinduliwa chama  kipya cha kisiasa  nchini kunatoa  fursa  ya    mashindano ya maoni   ya  kisiasa. Gazeti  linasema kuundwa chama  kipya  cha  kisiasa nchini  Afrika  kusini ni fursa kwa wapiga kura   ya kutafuta  njia mbadala nchini humo .

Gazeti linasema hiyo ni  changamoto kubwa    kwa chama  kinachotawala sasa-ANC.


Gazeti  la Berliner Morgenpost linazumngumzia   rais mteule wa Marekani  Barack Obama.

Linasema Obama  anaonekana kama rais wa   dunia nzima, lakini hali halisi, imo ndani  ya   nchi  yake.

Mhariri wa  gazeti la Berliner Morgenpost anaeleza kuwa  jambo  la kipaumbele kwa  Obama  sasa  ni kuimarisha mamlaka  yake  ndani  ya Marekani. Mtihani wake  wa  kwanza  utakuwa mnamo mwaka wa 2010  ambapo uchaguzi wa  bunge  utafanyika. Gazeti linatilia   maanani lengo la  Obama  juu ya kuhakikisha wingi wa wajumbe  wa chama  cha  Demokratik  kwenye seneti na kwenye  baraza la  wawakilishi.

Gazeti la  Schwäbische  Zeitung pia linazungumzia juu  ya  dhamira ya  rais meteule  Obama  juu ya kuleta sera mpya katika kukabiliana  na  mabadiliko ya hali ya hewa.

Gazeti hilo linasema  dhamira  ya Obama  imethibitika  katika uteuzi wa waziri  mpya  wa  nishati Steven  Chu. Mhaariri  wa  Schwäbische   Zeitung anaeleza  kuwa  kuteuliwa  kwa  waziri huyo  mpya bwana  Chu  kunaimarisha matumaini  juu  ya  dhamira  ya  rais mteule Barack  Obama  katika kukabiliana  na janga  la   mabadiliko  ya hali ya  hewa. Gazeti  linatilia  maanani kuwa waziri Chu ni mtetezi  wa mabadiliko  yanayokusudiwa  kuletwa  na Barack  Obama.Lakini hayo yataonekana kwenye  mkutano  wa  kilele  juu  ya hali ya hewa  utakaofanyika mjini Kopenhagen  mwaka  ujao.