Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani. | Magazetini | DW | 24.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Katika maoni yao, wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya kuuawa kwa wanajeshi watatu nchini Afghanistan.

Wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya kuuawa kwa askari watatu wa nchini Afghanistan.

Mhariri wa gazeti la Badische Neueste Nachrichten anasema askari wa Ujerumani waliopo nchini Afghanistan wanahitaji vifaa madhubuti vya kisasa.

Mhariri wa gazeti hilo anasisitiza hoja yake kwa kusema kuwa kwa muda wa miaka kadhaa wanajeshi wa Ujerumani waliopo nchini Afghanistan wamekuwa wanakataliwa ombi la kupatiwa silaha za kisasa kwa madai kwamba hatua hiyo ingetoa picha ya ushari wa kijeshi wa hali ya juu.

Juu ya mkasa wa askari hao watatu gazeti la Berliner Morgenpost linasema pana haja ya kusema ukweli juu ya jukumu la askari wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Kwa muda mrefu sehemu ya kaskazini mwa Afghanistan ilikuwa inaaminika kuwa tulivu, lakini hali sasa imethibi kuwa nyingine. Kutokana na ukweli huo siyo sahihi kwa waziri wa ulinzi kusema kwamba jukumu la askari wa Ujerumani nchini Afghanistan ni la kuimarisha utengemavu tu. Gazeti la Berliner Morgenpost,linasema mtazamo huo haueleweki kwa wanajeshi,na kwa wananchi wengine kadhalika.

Mhariri wa gazeti la Sächsische anaunga mkono hoja hiyo kwa kusema kwamba kutumia kauli zilizonakshiwa juu ya hali ya nchini Afghanistan kunachangia katika maafa kama hayo.Mhariri huyo anasema askari yeyote aliepo nchini Afghanistan yupo vitani.

 • Tarehe 24.06.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IYED
 • Tarehe 24.06.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IYED