Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani. | Magazetini | DW | 02.09.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Katika maoni yao wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wanazungumzia hasa juu ya mkutano maalumu wa viongozi wa Umoja wa Ulaya juu ya mgogoro wa Georgia.

Rais Sarkozy wa Ufaransa kwenye kikao cha dharura cha viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels.

Rais Sarkozy wa Ufaransa kwenye kikao cha dharura cha viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels.

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani karibu yote leo wanazungumzia juu ya mkutano maalumu wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya kuhusu mogogoro wa Georgia uliofanyika jana mjini Brussels....

Lakini wahariri hao pia wamezungumzia juu ya hatua ya benki ya Commerz kuinunua benki ya Dresdener. Wahariri wa magazeti pia hawakusahau kutoa maoni yao juu ya mkutano mkuu wa chama cha Republican nchini Marekani.

Juu ya kikao maalumu cha viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya gazeti la Lausitzer Rundschau linasema jambo muhimu ni kwamba kikao hicho kilifikia lengo lake- yaani kuzungumza kwa kauli moja. Lakini mhariri wa gazeti hilo anasema ,kuzungumza kwa sauti moja tu hakutoshi. Kinachotakiwa ni kuzungumza kwa kauli ya uwazi. Hatua ya kijeshi iliyochukuliwa na Georgia, haikuwa ya busara na ilisababisha vita.

Kwa hiyo, sasa ikiwa Georgia inataka kusaidiwa na nchi za Umoja wa Ulaya inapaswa kufuata shabaha zinazolengwa na Umoja huo. Aidha mhariri wa Lausitizer Rundschau anautaka Umoja wa Ulaya utoe kauli ya uwazi kwa wahusika wengine, na hasa Marekani, kwamba nayo pia inapaswa kutimiza wajibu wake. Lakini gazeti la Offenburger Tageblatt linasema Umoja wa Ulaya unadhibitiwa na maslahi ya kila mwanachama binafsi. Na matokeo yake ni maafikiano ya upeo wa chini katika ngazi ya kimataifa.

Gazeti la Westfalen Post linatoa maoni juu ya hatua ya benki ya Commerz kuinunua benki ya Dresdener. Mhariri wa gazeti hilo analalamika kuwa hatua hiyo itateketeza nafasi za ajira alfu sita na mia tano nchini Ujerumani pekee, na matawi ya benki 350 yatafungwa.

Lakina katika upande mwingine gazeti la Rhein Zeitung linafurahi kwamba benki ya Dresdener imenunuliwa na benki ya Commerz, badala ya kumezwa na benki ya serikali ya China.


Mhariri wa gazeti la Frankfurter Rundschau anaesema ,kwamba kwa kujaribu kuweka kando maslahi yake ,ili kushikamana na watu wanaokabiliwa na madhara ya kimbunga Gustav, chama cha Republican asilani hakijiongezei sifa, kutokana na utobwe alionesha rais Bush, wakati wa kimbunga Katrina.


Conclusion... • Tarehe 02.09.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F9lw
 • Tarehe 02.09.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F9lw