1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya Ukraine

Abdu Said Mtullya16 Aprili 2014

Wahariri wa magazeti wanazungumzia juu ya mgogoro wa Ukraine na juu ya biashara ya silaha kati ya Ujerumani na Saudi Arabia

https://p.dw.com/p/1BiMm
Rais wa mpito wa Ukraine Oleksandr Turchynov akikagua gwaride la kijeshi
Rais wa mpito wa Ukraine Oleksandr Turchynov akikagua gwaride la kijeshiPicha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Juu ya mgogoro wa nchini Ukraine gazeti la "Die Rheinpfalz" Ukraine linavizungumzia vikwazo viliyvowekwa na nchi za magharibi ili kumwadhibu Rais Vladimir Putin wa Urusi.

Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa vikwazo vinaweza kumfanya mlengwa aibadilishe tabia yake, lakini haviwezi kuleta miujiza. Mhariri huyo anasema matumaini kwamba vikwazo vinaweza kumfanya Putin aubadilishe kabisa msimamo wake juu ya Ukraine yamo katika msingi wa dhana tu.

Mhariri wa gazeti la "Die Rheinpfalz" anasema ipo mifano mingi inayoonyesha ,kwamba vikwazo havikuleta manufaa yoyote.

Matayarisho hafifu

Mhariri wa gazeti la "Darmstädter Echo" pia anazungumzia juu ya mgogoro wa Ukraine. Na anasema kwamba nchi za magharibi hazikuwa zimejitayarisha vizuri ili kuukabili mgogoro huo. Mhariri wa gazeti hilo anasema nchi za Ulaya zingeliwasiliana na Marekani na kukubaliana juu ya kuitayarisha orodha ya vikwazo, na kuviweka hatua kwa hatua,baada ya Urusi kulichukua jimbo la Krimea na kuliingiza katika himaya yake.

Lakini sasa nchi za Ulaya zinasuasua na badala yake zinatoa maelezo juu ya mkutano unaotarajiwa kufanyika Alhamisi ambapo Urusi pia itashiriki. Viongozi wa Ulaya wanakuliana kwamba Urusi ndiyo ya kulaumiwa kwa kushtadi kwa mgogoro nchini Ukraine.Lakini msimamo huo pekee hautoshi kumzuia Putin na wala hautoshi kuiokoa Ukraine.

Kura ya maoni ni ujasiri wa Rais wa mpito nchini Ukraaine au pata potea?


Gazeti la "Braunschweiger " linauzingatia ujasiri wa Rais wa kipindi cha mpito nchini Ukraine wa kujaribu kuitisha kura ya maoni katika majimbo ya mashariki mwa Ukraine. Mhariri wa gazeti hilo anafafanua kwa kusema ikiwa kaimu Rais Turchynov atakuwa sahihi juu ya mpango wake, na ikiwa kweli shauku ya kutaka kujiunga na Urusi itakuwa ndogo miongoni mwa , watu mashariki mwa Ukraine, basi hoja ya kujitandaza ya Rais Putin wa Urusi, haitakuwa na mashiko.

Lakini ikiwa Kaimu Rais wa Ukraine, Bwana Turchynov anajidanganya, basi huo ndio utakuwa mwanzo wa kumegekamegeka kwa nchi ambayo leo inaitwa Ukraine.

Vifaru vya Ujerumani kwa Saidi Arabia

Shirika la utafiti wa masuala ya usalama,SIPRI limetoa ripoti juu ya bajeti za kijeshi duniani. Mhariri wa gazeti la "Badische" anatoa maoni yake juu ya ripoti hiyo kuhusiana na Saudi Arabia.

Anasema bajeti ya kijeshi ya Saudi Arabia iliongezeka kwa asilimia 14 mwaka uliopita, na sasa nchi hiyo inataka kuvinunua vifaru kutoka Ujerumani. Hayo yanathibitisha kwamba nchi hiyo inawania kuwa na nguvu za kijeshi ili kuzipita nchi nyingine zote katika eneo lote la Arabuni.Viongozi wa nchi hiyo hawazijali haki za binadamu.

Ni kutokana na sababu hiyo kwamba Waziri wa uchumi wa Ujerumani anapaswa kuutilia mashaka mpango wote wa kuiuzia Saudi Arabia vifaru vya Ujerumani.

Mwandishi:Mtullya Abdu./Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Yusuf Saumu