Maoni ya wahariri juu ya ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa Jerusalem. | Magazetini | DW | 04.12.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa Jerusalem.

Wahariri wanatoa maoni juu ya uamuzi wa Netanyahu kujenga maakazi zaidi ya walowezi, na utatanishi unaotokana na baishara ya silaha baina ya Ujerumani na Saudi Arabia.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Mhariri wa gazeti la "Mitteldeutsche" anasema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.Mhariri huyo anatilia maanani kwamba mkutano huo ni baina ya marafiki. Lakini anasema, katika diplomasia hata marafiki, wanapaswa kusema mambo ambayo si ya kirafiki.Mhariri huyo anaeleza kuwa uamuzi wa kujenga maakazi zaidi ya walowezi umesababisha malalamiko katika nchi nyingi. Marafiki wa Israel wametambua kwamba,anachokifanya Waziri Mkuu Netanyahu kinawachochea maadui wa Israel.

Gazeti la "Badische" pia linaitaka serikali ya Ujerumani izungumze na Netanyahu juu ya ujenzi wa maakazi mapaya Mhariri wa gazeti hilo anasema itakuwa vizuri kwa Ujerumani, kumkazia macho rafiki yake Israel, na kumwambia Waziri Mkuu wa nchi hiyo Netanyahu kwamba anachokusudia kukifanya hakitaleta manufaa kwa nchi yake, ikiwa Wapalestina hawatayaona matumaini juu ya kuwa na nchi yao huru.

Mhariri wa "Frankfurter Algemeine" anasema tangazo la Israel juu ya kujenga makaazi mapya 3000 Mashariki mwa Jerusalem ,halichangii katika juhudi za kuleta suluhisho la amani katika Mashariki ya Kati. Ujenzi wa maakazi hayo utakiuka sheria za kimataifa.

Gazeti la"Sächsiche" linatoa maoni juu ya biashara ya silaha baina ya Ujerumani na Saudi Arabia.Linaitahadharisha serikali ya Ujerumani juu ya hatari ya kukiuka haki za binadamu . Mhariri wa gazeti hilo anasema, mtu anaingiwa wasiwasi kwamba huenda vifaru vya kisasa vitakavyouzwa kwa Saudi Arabia vikatumiwa kwa ajili ya kuwanyamazisha wapinzani katika nchi ya jirani.Biashara ya silaha ni jambo nyeti . Na kwa hivyo ni lazima idhibitiwe na watu wengi badala ya kikundi kidogo cha watu.

Mhariri wa "Stuttgarter" anasema haina maana kwamba kila mauzo ya silaha ni jambo baya wakati wote Lakini jambo baya ni ukosefu wa uwazi katika biashara hiyo.

Gazeti la "Lübecker Nachrichten" linatahadharisha juu ya ahadi iliyotolewa na kamishna wa masuala ya kijamii wa Umoja wa Ulaya juu ya kuwapatia ajira vijana wote wasiokuwa na kazi katika Umoja wa Ulaya katika kipindi cha miezi minne ijayo. Mhariri wa gazeti hilo anasema yeyote anaetoa ahadi kama hiyo,kana kwamba kupata ajira ni jambo la kijana kuamua tu, kufanya kazi, mtu huyo anapuuza hali halisi. Katika mazingira ya sasa ya mgogoro wa madeni, kutoa ahadi kama hiyo kunaweza kusababisha masikitiko baadae.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen:

Mhariri: Mohammed Khelef