MAONI YA WAHARIRI JUU YA UAMUZI WA MAHAKAMA KUU YA UJERUMANI. | Magazetini | DW | 08.09.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

MAONI YA WAHARIRI JUU YA UAMUZI WA MAHAKAMA KUU YA UJERUMANI.

Wahariri wa magazeti leo wanatoa maoni yao juu ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Ujerumani kuhusu kuzisaidia nchi zenye madeni barani Ulaya.

default

Mahakimu kwenye Mahakama Kuu ya Ujerumani mjini Karlsruhe.

Suala linalozunguziwa na wahariri leo zaidi kuliko jingine lolote ni uamuzi wa Mahakama Kuu ya Ujerumani uliotelewa jana kusema kwamba kushiriki kwa serikali ya Ujerumani katika kuzisaidia nchi zenye madeni katika Umoja wa sarafu ya Euro ni sahihi kisheria.

Mhariri wa gazeti la Hannoversche anasema endapo Mahakama Kuu ingeulitoa uamuzi mwingine,serikali ya Ujerumani ingelipata fedheha na pia ingelikuwa ishara ya maafa kwa masoko ya fedha .Lakini Mahakimu wa Mahakama Kuu ya Ujerumani wametoa uamuzi unaosema kwamba sheria inayoiwezesha serikali ya Ujerumani kuzisaidia nchi zenye madeni katika Umoja wa sarafu ya Euro,inaenda sambamba na katiba ya nchi.

Lakini katika uamuzi wake, Mahakama hiyo pia imesisititiza kwamba Bunge la Ujerumani linapaswa kuwa na usemi mkubwa katika maamuzi yanayohusu kuzisaidia nchi zenye matatizo ya madeni katika Umoja wa sarafu ya Euro. Juu ya hayo gazeti la Mitetteldeutsche linaeleza kuwa sasa ni wazi kwamba serikali ya Ujerumani haiwezi kuwasha na kuzima jinsi ipendavyo. Na hiyo ni hatua nzuri, kwa sababu pamekuwapo na hatari ya serikali hiyo ya kujitumbukiza katika patapotea zinazochezwa na serikali za nchi nyingine. Kwa hiyo mhariri wa gazeti hilo anasema uamuzi ulitolewa jana na Mahakama Kuu ya Ujerumani pia ni onyo kwa wale wote waliopo kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya wanaotaka kuendelea kulundika viwango vikubwa vya fedha katika mfuko unaotumika kwa ajili ya kuzisaidia nchi zilizolemewa na mzigo wa madeni.

Naye mhariri wa gazeti la Flensburger anaongezea kwa kusema kwamba uamuzi wa Mahakama Kuu ya Ujerumani ni wa busara, kwa sababu kuanzia sasa bunge litakuwa na usemi mkubwa juu ya maamuzi yote yatakayohusu kuzisaidia nchi zenye madeni katika umoja wa sarafu ya Euro.

Rais Obama leo anatarajiwa kutoa hotuba muhimu bungeni juu ya kukabiliana na ukosefu wa ajira. Lakini mhariri wa gazeti la Financial Times Deutschland anasema ni jambo la mashaka iwapo Obama ataweza kuyatimiza matumaini ya wananchi wake. Tatizo ni kwamba anayokusudia kuyatimiza yatakabiliwa na vizingiti vingi vya kisiasa. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa Obama anakusudia kuekeza kiasi cha dola Bilioni 300 kwa ajili ya kutenga nafasi za kazi, lakini njia iliyopo kwake katika kuutekeleza mpango huo ni nyembamba. Gazeti la Financial Times Deutschland linasema kilichobakia kwa Obama sasa ni kujaribu kupita katika njia hiyo bila ya kupepesuka!

Mhariri wa Wetzlarer Neue Zeitung anazungumzia juu ya mwaka wa kumi tokea kufanyika mashambulio ya kigaidi.Anasema, licha ya kuwa dola Kuu Marekani pia imeshambuliwa na magaidi. Lakini chini ya uongozi wa Obama Marekani imejifunza kuepuka majikwezo. Ushuhuda ni uamuzi wa kuwarejeshea mamlaka watu wa Irak na wa Afghanistan kuziongoza serikali zao wao wenyewe.

Mwandishi/Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen

Mhariri/Josephat Charo

 • Tarehe 08.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12UvX
 • Tarehe 08.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12UvX