Maoni ya wahariri juu ya mkutano wa Waprotestanti | Magazetini | DW | 02.05.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya mkutano wa Waprotestanti

Magazeti yanatoa maoni juu ya mkutano mkuu wa 34 uliowaleta pamoja Wakristo wa madhehebu ya kiprotestanti kutoka Ujerumani na nje.

Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki,Askofu Mkuu Robert Zollitisch

Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki,Askofu Mkuu Robert Zollitsch

Gazeti la"Weser-Kurier" linatilia maanani kwamba mkutano huo bado unaendelea kuwa na mvuto. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba wakati akiba za benki za kanisa zinaendelea kukauka,mkutano huo mkuu unaendelea kuwavutia watu ,kutoka ndani ya Ujerumani na kutoka duniani kote na hasa vijana.

Gazeti la "Weser Kurier" linasema vijana hao wapo kwenye mkutano huo siyo kama wageni bali kama watu waliojizatiti katika masuala ya kanisa. Hata hivyo gazeti hilo linatoa ushauri kwa Kanisa, kujaribu kutafuta njia mpya za kuwavutia waumini zaidi.

Malalamiko ya Makasisi:

Mhariri wa "gazeti la "Die Welt"anayatilia maanani malalamiko yanayotolewa na makasisi juu ya washiriki wa mkutano. Mhariri huyo anaeleza kwamba kwenye mkutano huo mkuu wa Waprotestanti mjini Hamburg, washiriki wanayajadili kwa mapana na marefu masuala ya mgogoro wa fedha,ulinzi wa mazingira na njia za kuwashirikisha wote katika neema ya jamii. Mkutano huo unaohudhuriwa na washiriki karibu laki moja pia ni mahala pa elimu ya siasa kwa umma.

Hata hivyo makasisi wanalalamika kwamba Mwenyezi Mungu anazingatiwa kuwa ni chanzo cha nguvu ya kutoa baraka bila ya kuchagua .Lakini inapohusu kumwabudu, ni watu wachache tu wanaofunga sala.

Gazeti la "Kieler Nachrichten "linawataka washiriki wa mkutano wa mjini Hamburg wamwombee Uli Hoeneß katika sala zao, kwa sababu mkutano wa Wakristo hao unafanyika pia chini ya kauli mbiu inayosema "Jee ni nini hasa anachokihitaji binadamu ili kuishi? Uli Hoeneß ambaye ni Rais wa timu ya kandanda ya Bayern Munic anakabiliwa na tuhuma za kukwepa kulipa kodi

Obama kuifunga jela ya Guantanamo.?

Gazeti la"Braunschweiger"linatoa maoni juu ya jela ya Guantanamo.

Linasema baada ya miaka minne na nusu katika Ikulu, Rais Obama amesema anataka kuifunga jela ya Guantanamo.Lazima patakuwa na sababu kubwa ya msingi. Wanapokuwamo katika muhula wa pili wa Urais, Marais wa Marekani wanakuwa makini sana juu ya historia. Hiyo ndiyo sababu kwamba wanajaribu kukiondoa kinachoweza kuitia doa historia yao.

Rais Obama anakusudia kuliondoa dola la jela ya Guntanamo.Lakini pana mashaka iwapo atafanikiwa. Gazeti la "Frankfurter Rundschau" pia limeandika juu ya Rais Obama kuhusiana na mgogoro wa Syria.Mhariri wa gazeti hilo anasema Rais huyo yumo katika mtanziko kwa sababu Marekani haijui ifanye nini ili kuutatua mgogoro wa Syria.

Mwandishi:Mtullya abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Daniel Gakuba