1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya mkutano wa Syria

Abdu Said Mtullya22 Januari 2014

Wahariri wanatoa maoni juu mazungumzo ya kuutatua mgogoro wa Syria yaliyoanza katika mji wa Montreux nchini Uswisi.Jee pana matumaini ya mkutano huo kufanikiwa?

https://p.dw.com/p/1AvEy
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwenye mkutano juu ya Syria
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwenye mkutano juu ya SyriaPicha: Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Juu ya mkutano kuhusu kuutatua mgogoro wa Syria, mhariri wa gazeti la "Freie Presse" anasema ni bora kutumia maneno kuliko mizinga. Mhariri huyo anatilia maanani kwamba lengo la nchi za magharibi na la wapinzani wa Assad kwenye mkutano huo ni kuzungumzia juu ya kuundwa serikali ya mpito bila ya ushiriki wa Rais Bashar al -Assad.Mhariri huyo anasema msimamo huo utaukwamisha mkutano.

Mhariri wa gazeti la "Nurnberger Nachrichten" anakubaliana na hoja hiyo kwa kusema kwamba njia zote za kuleta suluhisho nchini Syria zinapitia kwa Assad. Mhariri huyo anaeleza kwa kwamba Assad bado anao uzito mkubwa katika mambo ya usalama. Aidha bado analo jeshi kubwa . Funzo la Iraq bado limo alikini mwetu."Tumeweza kuona katika nchi hiyo nini kinaweza kutokea ikiwa Dikteta anatimuliwa haste haste"

Gazeti la "Thüringischen Landeszeitung"linatilia maanani kwamba wakati mkutano wa mjini Montreux unaendelea,yametolewa madai juu ya kuteswa kwa mamia ya watu nchini Syria na utawala wa Assad.Mhariri wa gazeti hilo anasema madai hayo yanaonyesha jinsi pande zinazohusika na mgogoro wa Syria zilivyofarakana. Kutokana na hali hiyo matumaini ya kufanikiwa kwa mkutano huo ni madogo sana.

Uturuki na Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uturuki Erdogan ameenda makao makuu ya Umoja wa Ulaya ili kuwasilisha hoja juu ya nchi yake kujiunga na Umoja huo. Mhariri wa "Westfälische Nachrichten" anasema ziara ya Erdogan kwenye makao makuu ya huo inakumbusha tahadharri zilizotolewa na wapinzani wake kwamba,Waziri Mkuu huyo yumo katika njia ya kuutosa mustakabal wa nchi yake, Uturuki.

Kongamano la uchumi wa dunia

Gazeti la "Bild" linazungumzia juu ya kongamano la uchumi wa dunia lililoanza nchini Uswisi.Mhariri wa gazeti hilo anasema kinachotakiwa ni hatua thabiti za kuyafanya maisha ya watu yawe bora duniani kote-kinachotakiwa ni dunia ya haki na siyo jukwaa la manaeno matupu. Mhariri wa gazeti la "Bild" anasema "tunawataka washiriki wa kongamano wawe na macho ya kuyaona mambo vizuri"

Mwandishi:Mtullya Abdu./Deustche Zeitungen.

Mhariri: Josephat Charo