Maoni ya wahariri juu ya Misri na Ugiriki | Magazetini | DW | 18.07.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya Misri na Ugiriki

Wahariri leo wanatoa maoni juu ya hali ya nchini Misri baada ya kuundwa serikali. Pia wanaizungumzia Ugiriki katika muktadha wa ziara ya Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton akutana na Rais wa muda wa Misri Adli Mansour

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Ashton akutana na Rais wa muda wa Misri Adli Mansour

Gazeti la "Süddeutsche" linaitafakari hali tete ya kisiasa nchini Misri baada ya kuundwa serikali. Mhariri wa gazeti hilo anasema serikali hiyo imeundwa wakati ambapo Misri ipo katikati, ikivutwa baina ya pande mbili. Wale wanaomuunga mkono Rais alieondolewa madarakani na jeshi, Mohammed Mursi, na katika upande mwingine wale wanaompinga.

Serikali iliyoundwa ina watu wanaoshiria matumaini kama vile Mohammed ElBaradei. Yeye na rafiki zake ndiyo waliotoa mwito kwa jeshi- na kwa hivyo sasa wanapaswa kutawala pamoja na wanajeshi. Gazeti la "Süddeutsche " linasema matatizo ya Misri ni makubwa sana na subira ya wananchi ni ndogo.Na kutokana na hali hiyo ,serikali mpya inapaswa ianze kazi mara moja.

Ziara ya Schäuble nchini Ugiriki:

Gazeti la "Neue Osnabrücker " linaizungumzia ziara ya nchini Ugiriki ya Waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble anayoifanya wakati mihemko ya watu ni ya juu. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kuwa Waziri Schäuble hatapokewa kwa moyo mkunjufu.

Mhariri anaeeleza kuwa ni wazi,kwamba atakutana na Waziri mwenzake na pia na Waziri Mkuu wa Ugiriki kwa ajili ya mazungumzo.Lakini nje ya chumba cha mazungumzo wapo watu wanaosubiri wakiwa wamejawa hasira vifuani.

Watumishi wa Umma wamekuwa wanafanya maandamano kutokana na kuhofia kuachishwa kazi. Lakini hayo ndiyo masharti ambayo Ugiriki inapaswa kuyatimiza. Na haina njia nyingine. Waziri Schäuble anaiunga mkono njia hiyo.

Wananachi wa Ujerumani wakasirishwa:

Gazeti la "Tagesspiegel" linatoa duku duku lake lote kwa serikali ya Ujerumani juu ya kashfa ya upelelezi.

Gazeti hilo linuliza jee pana haja gani ya kuwa na serikali isiozitetetea haki za kimsingi. Mhariri wa gazeti hilo anasema ni jambo la kukasirisha sana, kwa Waziri wa mambo ya ndani, ambae anapaswa kuwa mlinzi wa katiba kusema kuwa yaliyofanywa na mashirika ya ujasusi ya Marekani siyo mambo mabaya sana. Lakini wakati huo huo waziri huyo anasema kuwa hajui kwa uhakika juu ya kilichotokea.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitunge.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman