Maoni ya wahariri juu ya Mashariki ya Kati | Magazetini | DW | 16.07.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya Mashariki ya Kati

Wahariri leo wanatoaa maoni juu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati, mabadiliko ya baraza la mawaziri nchini Uingereza na juu ya Rais mpya wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya.

Hamas yaendelea na mapigano

Hamas yaendelea na mapigano

Gazeti la "Weser -Kurier" linatilia maanani kwamba katika juhudi za kuutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amefanya ziara katika Mashariki ya Kati.

Mhariri wa gazeti la "Weser-Kurier"anasema hatua thabiti ya kuyasimamisha mapigano itaweza kufikiwa katika Mashariki ya Kati ikiwa tu, Hamas itaondoka Ukanda wa Gaza.Lakini hakuna mwenye ushawishi wa kuwezesha kufikiwa lengo hilo. Mhariri wa gazeti la "Weser-Kurier" anasema kwa kadri Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wanavyoendelea kuuliwa na mabomu ya Israel,ndivyo Hamas inavyoendelea kujijenga.

Ndiyo kusema Hamas itaendelea na mkakati wa kuishambulia Israel kwa roketi ili kuichokoza. Hivyo basi itakuwa vigumu kwa Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Steinmeier kukiondoa kizungumkuti hicho.

Hakuna anaetaka amani

Gazeti la "Nürnberger Nachrichten" linatilia maanani kwamba pande zote mbili hazipo tayari kuyasimamisha mapigano na linaeleza kwamba wakati Israel inatoa mwito kwa Wapalestina wa Gaza waondoke kwenye makaazi yao ,Hamas inawataka watu wa Ukanda wa Gaza wajitoe mhanga na wawe tayari kufa mashahidi. Katika hali kama hiyo itakuwa vigumu kuleta amani au angalau kuyasimamisha mapigano.

Cameron awatimua wapinzani


Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.Gazeti la "Neue Osnabrücker" linajiuliza, jee alichokifanya Cameron ni kitendo cha busara au upumbavu?

Mhariri wa gazeti hilo anafafanua kwa kusema kwamba Cameron amesimama mbele ya mambo matatu muhimu.Kura ya maoni katika Scotland,uchaguzi wa Bunge mwakani na kura ya maoni juu ya kuamua iwapo Uingereza iendelee kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Na Kwa hivyo hana njia nyingine ila kuwaondoa wale wanaompinga katika baraza lake la mawaziri.

Hatahivyo ikiwa watu nchini Uingereza watabainisha kwamba lengo lake katika kuwaondoa mawaziri fulani ni kuyaimarisha mamlaka yake basi ataonekana kama mtu anaepiga kelele za uoga.

Jee Juncker atauboresha Umoja wa Ulaya ?

Jean - Claude Juncker amethibitishwa kuwa Rais mpya wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya. Mhariri wa "Frankfurter Neue Presse" anatoa maoni yake kwa kusema sasa bwana Juncker anapaswa kuthibitisha kwamba anaweza kuufanya Umoja wa Ulaya uwe bora zaidi.

Jambo muhimu kabisa kwake ni kuonyesha jinsi atakavyoyagawa majukumu ya Halmashauri yake.Idara imara zinahitajika ili kuyashughulikia masuala muhimu kama vile ya fedha,ugavi wa nishati,ulinzi ya mazingira na wakimbizi.Katika masuala hayo panalazimu utangamano mkubwa zaidi wa Ulaya.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman