1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Uwanachama wa Umoja wa Ulaya sasa ubadilike

Mohammed Khelef
24 Juni 2022

Sababu za kutanuka kwa Umoja wa Ulaya zinabadilika. Kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, sasa siasa za kikanda zinahitajika zaidi kuamua utanukaji huo kuliko majadiliano kama ya Balkan, anaandika Bernd Riegert.

https://p.dw.com/p/4DCqI
Belgium EU Summit Western Balkans
Picha: Olivier Matthys/AP/picture alliance

Fadhaa ni kubwa miongoni mwa waombaji wa hivi karibuni wa uwanachama wa Umoja wa Ulya katika mataifa ya Balkan Magharibi. Yameahidiwa uwanachama kwa miongo kadhaa sasa, lakini hakujakuwa na maendeleo yoyote kutokana na sababu kadhaa wa kadha. Ghafla moja, Ukraine na Moldova zinakuja juu kuyapiku mataifa ya Balkan Magharibi. Zimepatiwa ugombea uwanachama kufumba na kufumbua.

Fadhaa hii ni jambo la kueleweka, lakini imejikita kwenye dhana za uwongo. Utanukaji wa Umoja wa Ulaya utahusiana na siasa za kikanda, utahusiana na kukabiliana na hamu ya kibeberu ya rai swa Urusi. Tafauti na ilivyo kwenye Balkan Magharibi na kwa kiwango kikubwa pia suala maalum la Uturuki, hili sio tena suala la kuzingatia vigezo vya kisiasa na kiuchumi katika kuzikubalia uwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Bahati nasibu ya lazima

Kwa uamuzi huu wa kihistoria wa kulichukuwa taifa kubwa kabisa lililosambaratishwa kwa vita, Umoaj wa Ulaya imeweka vigezo vipya kabisa. Hii ni bahati nasibu ya kisiasa, anasema waziri wa mambo ya kigeni mwenye uzoefu mkubwa, Jean Asselborn wa Luxembourg. Bahati nasibu ya lazima. Wale wanaotaka kucheza bahati nasibu isiyo na hatari nyingi, kama vile Ufaransa, Uholanzi, Ureno na pia Ujerumani, wanajifariji wenyewe kwa ukweli kwamba hatua hii haigharimu chochote leo na kwamba, baada ya miaka kadhaa ya majadiliano, uwezekano halisi wa Ukraine kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya bado ni jambo lisilo hakika huko twendako.

Katika muda wa kati na kati, hatua hii ya kihistoria itakuwa pia na athari kwenye kukubaliwa uwanachama wa mataifa mengine ya Balkan. Kwa kuwa kwa sasa Umoja huo kwa sasa kimsingi unashughulishwa Zaidi na kuurejesha nyuma ushawishi wa Urusi na China katika eneo hilo. Vigezo vya kujiunga, ambavyo awali vilikuwa lazima vizingatiwe kwa undani, sasa vitakuwa rahisi kwa kiasi fulani.

Tabia ya kukera na isiyo ya maana ya Bulgaria kupiga kura ya kuzuwia mara kwa mara lazima sasa ikomeshwe haraka. Si jambo linalokubalika kwa nchi moja ya Umoja wa Ulaya kutumia matatizo yake ya ndani ya kisiasa kuuchukuwa mateka mchakato wa kujiunga na Umoja huo. Lakini hilo si kwa Bulgaria, bali pia kwa Ugiriki na Ufaransa ambazo zimepigia kura ya turufu katika wakati muhimu sana wa Umoja wa Ulaya.

Mataifa ya Balkan lazima yatatuwe matatizo yao wenyewe

Hata hivyo, matatizo ya njia za awali za kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa mataifa ya magharibi mwa Balkan kwa kiasi kikubwa yanakwendana na Umoja wenyewe. Vikwazo vikubwa hasa lazima vitatuliwe na waombaji wenyewe: demokrasia makini, utawala wa sehria, utatuzi wa mizozo na majirani zao. Hivi haviwezi kufanywa wala kuagizwa na Umoja wa Ulaya. Mataifa hayo yanapaswa kujifanyia wenyewe. Bosnia-Herzegovina, Kosovo, Serbia na Albania bado zina kazi ya kufanya.

Lingelikuwa jambo jema ikiwa nchi 26 za Umoja wa Ulaya zingeishinda nguvu Bulgaria na kuanza mazungumzo ya kujiunga na Umoja huo na Marcedonia Kaskazini na Albania. Lakini kwa bahati mbaya, msingi wa ridhaa ya wote ilizuwia hilo. Kwa maana hiyo, mkutano wa kilele mjini Brussels kwa mara nyengine tena ulipoteza fursa  hii muhimu ya kuanza juudi za kuyaelekea mataifa ya balkan Magharibi. 

Lakini inatuma ujumbe mkali kwa Urusi: licha ya ugumu wote, Umoja wa Ulaya uko tayari kuchupa kivuli chake na kuichukuwa Ukraine kuwa mwanachama wake. Na Moscow haiwezi kulizuwia hilo.

Bernd Riegert Brüssel
Bern RiegertPicha: DW