1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ni: Serikali ya umoja ni hatua ya kwanza Sudan Kusini

27 Aprili 2016

Katika maoni yake mwandishi mwalikwa, Henrik Maihack kutoka wakfu wa Friedrich- Ebert anasema kurejea kwa Machar ni hatua ya kwanza katika juhudi za mgogoro wa nchini Sudan Kusini.

https://p.dw.com/p/1IdMt
Viongozi wa Sudan Kusini,Rais Salva Kirr na Makamu wake Riek Machar
Viongozi wa Sudan Kusini,Rais Salva Kirr na Makamu wake Riek MacharPicha: Getty Images/AFP/S. Bol

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar hatimaye amerejea nchini na kushika wadhifa wa Makamu wa Rais .Serikali ya umoja ni hatua ya kwanza ya kuleta amani nchini Sudan Kusini. Ndiyo sababu utulivu wa kudumu unapaswa kuleta manufaa makubwa zaidi kuliko mapambano ya mtutu wa bunduki .

Kiongozi wa waasi Riek Machar hatimaye amerejea nchini baada ya kuchelewa kwa muda wa wiki moja.

Mwandishi wa maoni Henrik Maihack kutoka Wakfu wa Friedrich Ebert
Mwandishi wa maoni Henrik Maihack kutoka Wakfu wa Friedrich EbertPicha: Friedrich-Ebert-Stiftung

Kwanza alitaka kurejea na silaha na idadi ya askari kinyume na makubaliano .Na ndiyo sababu hakuruhusiwa na serikali kutua nchini. Kutokana na kuvunjika moyo Marekani ilitaka kugoma kugharimia safari yake.Hata hivyo Umoja wa Mataifa uliingilia kati na kumsafirisha Machar.

Hakika huo sio mwanzo mzuri

Mnamo mwaka 2013 Rais Salva Kirr alidai kwamba Makamu wake Machar alikuwa anakula njama za kuiangusha serikali.Na tokea wakati huo Sudan Kusini imezama katika damu.

Hata hivyo baada ya mazungumzo kadhaa, Machar aliukubali mkataba wa amani wakati akiwapo nchini Ethiopia Pamoja na vipengele muhimu vya mkataba huo ni kuundwa serikali ya umoja . Hiyo ni hatua muhimu.

Serikali hiyo itakuwa na jukumu la kuandaa mchakato wa katiba na maridhiano hadi utakapofanyika uchaguzi mnamo mwaka wa 2018. Kutokana na kila upande kutokuwa na imani na upande mwingine, ni vigumu kuona jinsi mchakato huo utakavyofanikiwa.

Katika sehemu nyingi za Sudan Kusini mapigano bado yanaendelea.Hivi karibuni tu watu zaidi ya mia mbili waliuawa kwenye mpaka baina ya Sudan Kusini na Ethiopia.

Kwa mujibu wa uchambuzi juu ya hali ya kisiasa na kiuchumi nchini Sudan Kusini, mahasimu wa kisiasa wakati wote wameweza kudhibiti raslimali za nchi kwa kuyatumia makundi yenye silaha.

Muda mfupi kabla ya uhuru kutangazwa Sudan Kusini, mapigano yalikomeshwa pale ilipowezekana kuyanunua makundi fulani yaliyokuwa na silaha. Na kutokana hali hiyo, kiasi kikubwa cha fedha za nchi kilitumika kwa ajili ya ulinzi.

Askari wa jeshi la ukombozi SPLA wawasili Juba
Askari wa jeshi la ukombozi SPLA wawasili JubaPicha: Imago/Zumapress

Lakini utulivu kwa njia hiyo utaweza kudumishwa ikiwa raslimali za kutosha zitakuwapo. Lakini sasa kutokana na bei ya mafuta kuanguka Sudan Kusini imo katika hali mbaya ya kifedha.Watu zaidi ya Milioni tano wa nchi hiyo wanategemea misaada.

Na hata ikiwa serikali ya umoja ni hatua ya kwanza,utulivu wa kudumu,utaletwa, Sudan Kusini ikiwa amani italeta manufaa makubwa zaidi, kuliko mapambano ya mtutu. Serikali ilichelewa kuchukua hatua za kiuchumi ili kuzuia mapigano .

Nchi mpya ya Sudan kusini ilishindwa kujibadilisha kutoka kwenye uongozi wa kijeshi wa zama za mapambano ya ukombozi na kuanzisha uongozi imara wa kiraia.

Mwandishi:Henrik Maihack

Mfasiri:Mtullya Abdu.

Mhariri:Yusuf Saumu