Maoni : Sera ya kigeni ya Ujerumani ni thabiti na mahiri | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Maoni : Sera ya kigeni ya Ujerumani ni thabiti na mahiri

Mwaka 2015 ulikuwa na changamoto kubwa kwa utulivu wa Ulaya na kanuni zake Ujerumani bila ya kutarajiwa imeonyesha uongozi thabiti na diplomasia mahiri anasema Melinda Crane.

Kansela Angela Merkel na waziri wake wa Mambo ya nje Frank Walter- Steinmeier.

Kansela Angela Merkel na waziri wake wa Mambo ya nje Frank Walter- Steinmeier.

Mapema mwaka 2014 viongozi watatu wa Ujerumani Rais Joachim Gauck,waziri wa mambo ya nje Frank Walter Steinmeir na waziri wa ulinzi Ursula von der Leyen wametaka nchi hiyo kuwajibika zaidi katika jukwaa la kimataifa.

Wataalamu na wanasiasa walijadili sera thabiti zaidi inapaswa iwe na taswira gani.Ilichukuwa takriban miaka mwili lakini hivi sasa tunajuwa.Katika kipindi cha mwaka 2015 Kansela Angela Merkel na waziri wa mambo ya nje Frank Walter Steinmeir walitowa darasa la kuvutia la sera mpya ya mambo ya nje ya Ujerumani.

Mizozo mitatu imetishia utengamano wa Ulaya ikiwa ni pamoja na Ujerumani katika hali ambayo ni nadra kushuhudiwa tokea mwaka 1945.Ikiwa ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya yenye majirani wengi Ujerumani ina maslahi makubwa kwa utulivu wa baada ya kipindi cha vita ambao unahakikisha kutokiukwa kwa mipaka ya taifa utulivu uliotibuliwa na unyakuaji wa jimbo la Crimea nchini Ukraine uliofanywa na Urusi pamoja na kuingilia kati mashariki mwa nchi hiyo.

Uchumi muhimu wa Ulaya likiwa kama bara kuu linalosafirisja nje bidhaa hutegemea uthabiti wa sarafu.Na kwa sababu zote mbili za siasa za kimaeneo na uchumi Ujerumani inanufaika sana na mfumo wa Schengen wa mipaka ya ndani ya bara hilo kuwa wazi mfumo ambao hivi sasa unayumbishwa kutokana na nchi za kusini mwa Ulaya kujenga uzio na kuta katika juhudi potofu za kuzuwiya uhamiaji.

Melinda Crane Mwandishi Mkuu wa masuala ya kisiasa DW.

Melinda Crane Mwandishi Mkuu wa masuala ya kisiasa DW.

Masuala yote hayo matatu ya mzozo nchini Ukraine,deni la Ugiriki na umoja katika kanda ya sarafu ya euro na wakimbizi Kansela Merkel amefuata mkondo na kuushikilia licha ya upinzani ndani na nje ya nchi.Vyombo vya habari vya Uingereza na Marekani vimekuwa vikizichukia sera zake za kubana matumizi lakini bado amechaguliwa kuwa Mtu maarufu zaidi kwa mwaka 2015 na jarida la Times na kufikia wahariri wake kumpongeza kwa kuingilia kati kuiwekea dhamana Ugiriki kwa masharti yake mwenyewe yalio makali.

Uongozi sio lazima uwe sawa na sera ya kigeni lakini ni sharti ambalo huhitaji dira kufanikisha lengo lake la msingi ambalo ni kuhakikisha usalama na kwa mamlaka kulitekeleza.Dira ya Merkel kuhusu usalama inazingatia uhalisia.Anajuwa kwamba iwapo Ulaya itabidi ienzi kile inachotetea uvumilivu, uhuru na utu lazima ijiandae kubadilika.Jarida la Times pia linampongeza Merkel kwa kusimama kidete dhidi ya ugaidi na kwa hima yake.

(Mwaka uliopita ulikuwa wa hamasa kubwa kwa waziri wa mambo ya nje Frank Walter Steinmier.Ili iweze kufanikiwa sera ya kigeni lazima ichanganishe dira ya mkakati na diplomasia mahiri ambayo kwa hilo Steinmeier amekidhi haja. Ameshirki katika mazungumzo ya hadi usiku wa manane kufanikisha makubaliano ya Minsk kuhusu mzozo wa Ukraine na kuinusuru Ugiriki na madeni pamoja na kutafuta suluhisho la kidiplomasia kwa mpango wa nyuklia wa Iran na mzozo wa Syria.)

Wakati mwaka ukikaribia kumalizika ni jambo lililo wazi kwa nguvu zake zote mtizamo wa Merkel na Steinmeier umeshindwa kulipatia ufumbuzi suala moja kuu lilioko njia panda.Sera ya nje ya Ujerumani ufanisi wake una kikomo vinginevyo inaambatana na juhudi za wazi na makini za Ulaya na funzo kwa hilo ni mzozo wa wakimbizi.

Mwandishi : Melinda Crane/ Mohamed Dahman

Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com