1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanzo mpya Burkina Faso na mtu anayefahamika

1 Desemba 2015

Rais mpya wa Burkina Faso ana kazi kubwa ya ujenzi mpya. Muhimu zaidi katika kazi hiyo ni kurekebisha uhalifu uliotokea wakati wa kipindi cha utawala wa mtangulizi wake.

https://p.dw.com/p/1HFUI
Burkina Faso Präsidentschaftswahl - Gewinner Roch Kaboré
Rais mpya wa Burkina Faso Roch Marc Christian KaborePicha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Ugumu hata hivyo anasema katika maoni ya Dirke Köpp uko kwake binafsi kwa kuwa aliwahi kushika nyadhifa katika serikali iliyopita.

Matokeo ya uchaguzi nchini Burkina Faso yanamfanya mtu awe na hisia tofauti. Kwa upande mmoja uchaguzi ulikuwa unafurahisha kuwaona watu wakiwa katika misururu mirefu wakisubiri kupiga kura kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 55, katika uchaguzi, ambao rais hajajulikana kabla. Zaidi ya nusu ya muda huu wa kusubiri alikuwa akitawala Blaise Compaore, kabla ya kuangushwa kutoka madarakani Oktoba 2014. Umma ulikataa kukubali , kwamba rais abadili katiba, ili abakia kwa muda mrefu zaidi madarakani.

Kwa upande mwingine lakini ushindi wa kishindo wa Roch Marc Christian Kabore unazusha maswali kadhaa.

Kwa nini ameshinda uchaguzi huu mwanasiasa ambaye kwa miaka mingi amekuwa katika mfumo wa utawala wa rais wa zamani Blaise Compaore? Hii inaweza kuwa alipata usaidizi mahali fulani. Je ushindi huo haukupangwa mapema? Mfumo wa utawala wa Compaore una nguvu kiasi gani bado nchini Burkina Faso?

Kwa uhakika , Kabore hakuchoka kusisitiza , kwamba ametalikiana na mfumo wa zamani. Lakini ni kweli hilo? Na wasaidizi wake sio wale watumishi wa zamani? Na ni jukumu gani Ufaransa ilichukua katika sera zake kuelekea Afrika, katika kile kinachofahamika kama " Francafrique", ambazo Compaore alikuwa akiziunga mkono kabla ya kuondoshwa madarakani?

Dirke Köpp
Mwandishi wa maoni Dirke KöppPicha: DW

Kabore anafahamika kwa muda mrefu kuwa muungaji mkono mkubwa wa Compaore. Aliwahi kuwa waziri mkuu na baadaye kwa muda wa miaka kumi alikuwa spika wa bunge. Pamoja na hayo Kabore alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha rais Compaore, cha "Congress for Democracy and Progress," Umoja wa demokrasia na maendeleo, CDP).

Na baada ya hapo ukatokea mtengano baina yao, kwa kuwa Kabore hakutaka kukubali Compaore arefushe muda wake madarakani.

Kuhusu sababu za Kabore kuonesha kutoridhishwa kwake, kuna maoni tofauti; baadhi wanasema kwamba , huenda ni sababu za kiutu. wengine hata hivyo wanasema, Kabore alikasirishwa, kwasababu mpango uliokuwapo ni kwamba atachukua nafasi ya Compaore.

ukweli uko wapi, ni vigumu kufahamu. Kabore binafsi anasema. anataka tu kuangalia mbele.

Kwa hilo anajisikia vizuri, kwa kuwa kuna kazi kubwa inayomsubiri.

Ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Burkina Faso ni tatizo kubwa, kwa kuwa theluthi mbili ya wakaazi wa nchi hiyo ni vijana chini ya miaka 18. Tatizo hili linahitaji kushughulikiwa kwa haraka.

Kwa miaka kadhaa nchi hiyo imekuwa katika nafasi ya mwisho katika kielelezo cha uchumi cha Umoja wa Mataifa, na hiyo pia ni changamoto kubwa. Moja kati ya mada nyingine kubwa

katika utawala wake lakini ni pamoja na maridhiano na watu kufuatwa na kukamatwa kwa ajili ya kuadhabiwa.

Muda wa utawala wa Compaore, pamoja na mapinduzi mara mbili katika miaka ya 2014 na 2015 unapaswa kufanyiwa kazi. Katika hilo kwa kuwa kuna hatari kubwa, kwamba yeye anakinga njia, akiwa kama waziri mkuu wa zamani, spika wa bunge na mkuu wa chama tawala. Na nchi hiyo inaweza ikawa kama ilivyokuwa hapo kabla.

Mwandishi: Dirke Köpp/ZR/Sekione Kitojo

Mhariri: Gakuba Daniel