Maoni: Mrithi wa Abe, Suga laazima aonyeshe uwezo wake | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.09.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Maoni: Mrithi wa Abe, Suga laazima aonyeshe uwezo wake

Waziri Mkuu mpya wa Japan anapanga kutoa kipaumbele kwa ukuaji, kukutana na mahasimu wa kikanda na kuimarisha upimaji wa virusi vya corona. Yoshihide Suga anakabiliwa na kazi ngumu, anasema Martin Fritz.

Ingawa amekuwa katibu wa baraza la mawaziri la Abe kwa miaka minane, Yoshihide Suga hakuonekana mwenye uwezekano wa kumrithi mkuu wake wa zamani kama waziri mkuu na kiongozi wa chama cha Liberal Democratic - hasa kwa kuungwa mkono na wingi wa wazi wa wanachama wa chama cha LDP.

Suga si maarufu sana nchini Japan, hatokei kwenye himaya ya kisiasa, wala hakuwa na ushawishi wowote ndani ya LDP, ambacho kimedhibiti siasa za ndani kwa miaka 65.

Kuchaguliwa kwake kama kiongozi wa chama na waziri mkuu kumefanikishwa na muungano wa nyuma ya pazia uliomuuza kama mgombea wa mwendelezo na utulivu.

Soma pia:Yoshihide Suga ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Japan 

Wafuasi wa Suga pia walikuwa na malengo machache ya kwao vichwani walipomuunga mkono: Katibu mkuu wa LDP na waziri wa fedha wa Japan Taro Aso, walitaka kubakisha nafasi zao, na Abe alitaka kuhakikisha kwamba hasimu wake wa muda mrefu ndani ya chama, Shegeru Ishiba, hawi kiongozi wa chama.

Martin Fritz, Journalist in Tokio

Mwandishi wa Martin Fritz mwenye makaazi yake mjini Tokyo.

Abe, ambaye alitangaza kujizulu ghafla mwezi Agosti, yumkini alikuwa amehisabu kwamba, akiwa na mshirika wa karibu zaidi serikalini, mahakama ingeachana na uchunguzi wa ripoti za rushwa wakati wa utawala wake.

Utawala mpya unaonekana kuwa tayari - siyo tu kwa sababu ya kuwa mamlakani, muoga mwenye miaka 71, ambaye anashikilia wadhifa wake kutokana na kuungwa mkono na Abe, Aso, Nikai na wafuasi wao.

Suga anapaswa kuwa na ujasiri na kuitisha uchaguzi mpya wa mapema mwaka huu. Kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa covid-19 kunakoshuhudiwa hivi sasa ni fursa nzuri.

Soma pia: Mchakato waanza kumpata waziri mkuu Japan

Zama za Anko Reiwa

Wakati Mfalme Akihito alipojiuzulu mwaka 2019, Suga alipewa jukumu la kutambulisha zama mpya ya ufalme kwa Japan. Utawala wa Mfalme Naruhito utaitwa "Reiwa," au uelewano mzuri, Suga aliliambia taifa. Na Wajapan walijibu kwa kumuita Katibu Mkuu huyo wa baraza la mawaziri "Anko Reiwa."

Kuna mashaka ya kweli kwamba Anko Reiwa ana utashi wa kazi yake mpya. Suga anahitaji ushindi usio na mashaka wa uchaguzi kuhama kutoka kibaraka na kuwa kiongozi huru.

Ni hapo tu ndiyo anaweza kuondoka kwene kivuli cha mkubwa wake wa zamani na kuachana na jukumu la waziri mkuu wa mpito. Vingevyo, kila wakati atakapokosea, anaweza kutarajia vigogo wa chama kumshambulia.

Soma pia: Mbio za kuwania nafasi ya waziri mkuu Japan zaanza

Suga alitengeneza mpango wa fedha wenye kuvutia ambao unahusisha kuendeleza mfumo wa kiuchumi wa Abe unaojulikana kama Abenomics. Mpango huo unaleta mantiki: Nguzo zake za sera nyepesi ya kifedha, sera rahisi ya nidhamu ya kifedha na mikakati ya ukuaji ndiyo zana za sasa na usimamizi wa kiuchumi.

Baada ya kushughulikia mdororo uliyosababishwa na janga, ameweka malengo ya kuufanya utawala kuwa wa kidijitali, kuyapa nguvu maeneo ya vijini na kuimarisha mifumo ya kijamii. Masuala ya kimuundo ambayo hayajashughulikiwa kwa miongo kadhaa sasa yanaweza kuangaziwa.

Mchoro wa mwelekeo wake

Abe alipendelea miradi ya kitaifa, kama vile kuweka usalama chini ya makao makuu na kubadilisha katiba ili kuruhusu ushiriki wa kijeshi nje ya nchi. Aliharibu miaka minane kwenye miradi hii na aliepuka masuala makuu ili asiwakasirishe wapigakura. Alijielekeza kwenye uchumi kwa wazo kwamba mifumo imara ya kifedha ingemruhusu kutekeleza malengo mengine ya kisiasa.

Soma pia: Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe atangaza kujiuzulu

Suga anaitazama sera ya kiuchumi, ambayo ina athari za moja kwa moja kwa raia, kama yake mwenyewe. Hata hivyo, katibu mzuri wa baraza la mawaziri hawi moja kwa moja waziri mkuu mwenye uwezo.

Chombo cha utawala kinaweza kusimamiwa kwa mkono wa chuma; Kusawazisha maslahi ya mamlaka kunahitaji ujuzi wa kidiplomasia na busara ya kisiasa. Suga anapaswa kuwazingatia pia wapigakura.

Soma pia: Japan yakumbuka miaka 75 ya bomu la atomiki Hiroshima

Kwa kukosa uzoefu wa kimataifa, anaweza kuchukuliwa mwanzoni kwenye jukwaa la kimataifa kama mtu dhaifu. Matendo yake hayaonekani kumpatia sifa nyingi nyumbani, ambako janga la virusi vya corona linatishia kumharibia.

Ikiwa tayari imerikodi vifo 1,400 mpaka sasa, serikali ya Abe, ambayo aliiwakilisha kama msemaji, haikuonyesha ufanisi. Ikiwa Suga hatokuwa makini, anaweza kuondolewa kwenye nafasi hiyo haraka kama alivyoipata.