Maonesho ya Radio na TV (IFA) Berlin yafunguliwa | Masuala ya Jamii | DW | 30.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Maonesho ya Radio na TV (IFA) Berlin yafunguliwa

Maonesho ya 2007 ya radio na Tv yanafunguliwa kesho mjini Berlin na yataendelea hadi septemba 5 yakitembeza zana za kisasa .

Maonesho ya radio na TV ya kimataifa-maarufu Ujerumani kwa jina la “FUNKAUSTELLUNG” au IFA, yanafunguliwa rasmi kesho mjini Berlin.Hata kabla kufunguliwa kwake, kuna matumaini makubwa kuwa sekta ya biashara ya vyombo vya radio na Tv-vyombo vya umeme-electronics-inazidi kustawi.

Wale walioweka matarajio hayo hawakukosea:

Maonesho ya radio na TV- ni maonesho ya ufundi wmpya na wa kisasa wa zana hizo nay ale ya mwaka huu 2007 yanamurika kuwa biashara ya sekta hii inazidi kuongezeka na kustawi.Mjini berlin, kuanzia kesho makampuni 1212 kutoka nchi 32 mbali mbali yatatermbeza zana zao mpya hadi Septemba 5.

Christian Göke, ndie meneja wa shirika linaloandaa maonesho haya mjini Berlin na anasema:

“Tumefaulu na sio tu ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2006 kupiga hatua mbele,bali pia imewezekana kuweka rekodi mpya katika maonesho haya.

Tuko mbele zaidi kidogo kuliko mwaka ulioweka rekodi hadi sasa wa 2005.Kinacho tufurahisha zaidi ni kuona, kuna muongezeko pia humu nchini.”

Gurudumu la kwanza linakuza bishara ya sekta hii ni TV.

Mabingwa wanakisia mnamo miaka ijayo ,Tv za kizamani milioni 40 zitabadilishwa na wateja kwa kununua zile za kisasa kabisa-flat-TV.

Hatahivyo, baada ya ununuzi mkubwa wa TV za aina hii mwaka uliopita wa kombe la dunia la kabumbu nchini Ujerumani, ununuzi wa TV za aina hii ulipungua kasi.

Dr.Rainer Hecker,mwenyekiti wa bodi ya Jumuiya ya viwanda vya zana za burdani ,mawasiliano na ufundi (GFU) anasema:

“Soko zima la zana za TV na radio limeongezeka kwa kima cha 4.9 %.Sehemu kubwa imechukuliwa na wateja wa kibinafsi.

Vyombo vya kuburdisha na mawasiliano vya umeme, vimeongeza sehemu yake ya biashara kwa kima cha 2.6 % tu.Na hapo yafaa kuangalia kwa jicho la kombe la dunia la kabumbu la mwaka jana.Hatahivyo, hata kwetu Ujerumani, kuna uwezekanao zaidi wa kukua biashara hii .”

Kwahivyo, inatarajiwa maonesho ya mwaka huu mjini

Berlin, yatastawisha zaidi biashara katika nusu ya pili ya mwaka huu.Mbali na zana mpya za TV,tawi hili latarajia pia kujionea maonesho ya zana mpya za “digital-camera”,”MPR players”-michezo ya video-videogames,simu za mkononi za aina mpya na “notebooks”.

Kima cha muongezeko katika sekta hii chatarajiwa kufikia 2% chenye thamani ya Euro bilioni 23.

Kuongezwa kwa kodi ya mauzo mwanzoni mwa mwaka huu kwa kweli, kulizorotesha biashara.

Ukumbi wa maonesho huko Berlin, mara hii umepanuka kwa masafa ya mita za mraba 104.000 –sawa na 10% zaidi ya eneo la hadi sasa.Hii ni rekodi mpya inayobainisha umuhimu unaoshikamanishwa na maonesho ya radio na TV-Funkausstellung kupindukia soko la Ujerumani na la nchi za Umoja wa Ulaya.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com