1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mansour ajaribu kuweka udhibiti wake Misri

7 Julai 2013

Rais mpya wa Misri ameanza kuimarisha madaraka yake na udhibiti wa mitaa hata wakati wapinzani wake wa chama cha Kiislamu wamesema kuwa mamlaka yake ni kinyume na sheria na wakidai rais Mursi arejeshwe madarakani.

https://p.dw.com/p/193Iz
Egypt's chief justice Adly Mansour delivers a speech during his swearing-in ceremony as the country's interim president in the Supreme Constitutional Court. in Cairo on July 4, 2013, a day after the military ousted and detained Mohamed Morsi following days of massive protests. The ceremony, which was broadcast live on national television, came after the military swept aside Morsi on Wednesday, a little more than a year after the Islamist leader took office. AFP PHOTO / KHALED DESOUKI (Photo credit should read KHALED DESOUKI/AFP/Getty Images)
Rais mpya wa Misri Adli MansourPicha: Khaled Desouki/AFP/Getty Images

Kuondolewa kwa Morsi madarakani kwa njia ya mapinduzi kumesababisha maandamano makubwa pamoja na mapambano ya mitaani kati ya makundi hasimu.

ELBaradei hatakiwi

Kuonesha hali ya mgawanyiko mkubwa unaomkabili kiongozi huyo asiye na uzoefu wa kutosha , Adly Mansour, ofisi yake imesema kuwa kiongozi anayependelea mageuzi Mohammed ElBaradei ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa mpito lakini kauli hiyo ilibadilishwa haraka baadaye na kusema kuwa mashauriano bado yanaendelea .

Mwanasiasa ambaye yuko karibu na ElBaradei amesema hatua hiyo ya kubadilisha uamuzi inatokana na upinzani kutoka kwa chama cha kihafidhina kinachofuata siasa kali zinazoegemea dini ya Kiislamu ambacho utawala mpya unataka kushirikiana nacho.

Egyptian supporters of the Muslim Brotherhood shout slogans during a rally in support with deposed president Mohamed Morsi (featured on the poster) on July 6, 2013 outside Cairo's Rabaa al-Adawiya mosque. Egypt's Islamists vowed further protests today to demand the army restore the country's first democratically elected leader, after a day of clashes which saw 26 people killed across the country. AFP PHOTO/MAHMUD HAMS (Photo credit should read MAHMUD HAMS/AFP/Getty Images)
Waandamanaji wafuasia wa rais wa zamani MorsiPicha: Mahmud Hams/AFP/Getty Images

Utawala wa Mansour , wakati huo huo , umeanza kujaribu kuondoa kile Morsi alichokijenga. Amemuondoa mkuu wa usalama wa taifa na mnadhimu mkuu wa ikulu ya nchi hiyo.

Viongozi wabaki korokoroni

Waendesha mashtaka, wakati huo huo , wameamuru viongozi wakuu wa chama cha Morsi cha udugu wa Kiislamu ambao wamewekwa kizuizini washikiliwe kwa muda wa siku 15 wakisubiri uchunguzi uendelee kuhusiana na kushambuliwa na kuuwawa kwa waandamanaji wanane wiki iliyopita.

Hakuna ghasia kubwa zilizoripotiwa kati ya waungaji mkono na wapinzani wa Morsi wakati pande hizo mbili zimejikusanya tena baada ya usiku wa mapambano makali ambayo yameufanya mji wa Cairo kuwa eneo la mapambano.

Egyptian supporters of the Muslim Brotherhood sit during a rally in support with deposed president Mohamed Morsi (featured on the posters) on July 6, 2013 outside Cairo's Rabaa al-Adawiya mosque. Egypt's Islamists vowed further protests today to demand the army restore the country's first democratically elected leader, after a day of clashes which saw 26 people killed across the country. AFP PHOTO/MAHMUD HAMS (Photo credit should read MAHMUD HAMS/AFP/Getty Images)
Wafuasia wa rais wqa zamani Morsi wakiendelea na maandamanoPicha: Mahmud Hams/AFP/Getty Images

Mapigano pia yamekuwa makali katika mji wa bandari wa Alexandria, ambako maelfu ya wafuasia wa kila upande walipigana kwa risasi, mabomu ya moto na virungu.

Ghasia za Ijumaa zimesababisha watu 36 kuuwawa, na kufikisha idadi ya karibu watu 75 waliouwawa tangu ghasia hizo kuzuka hapo Juni 30, wakati mamilioni ya waandamanaji wakiingia mitaani katika mkesha wa mwaka wa kwanza tangu Morsi kuingia madarakani kidemokrasia.

Morsi ambaye ni mhandisi aliyepata mafunzo yake nchini Marekani ambaye anashutumiwa sana na wakosoaji kwa kuhodhi madaraka binafsi na kwa ajili ya chama chake cha udugu wa Kiislamu pamoja na kushindwa kwake kutekeleza mageuzi ya kidemokrasia ya kiuchumi , ameendelea kubaki kizuwizini katika eneo ambalo halijilikani.

Senior opposition figure Mohamed El Baradei (R) and Leftist leader Hamdeen Sabahi stand during a news conference ahead of the planned protest against Egypt's President Mohamed Mursi, at the end of the month, in Cairo June 22, 2013. Anti-Mursi protests have been planned for June 30, when Mursi completes a first year in office marked by division and economic problems, by the president's opponents. REUTERS/Asmaa Waguih (EGYPT - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Mohammed el-Baradei (kulia)Picha: Reuters

Wasi wasi wazidi

Hali ya wasiwasi imeendelea kuongezeka wakati mamia kwa maelfu ya wafuasia wa Morsi wakiingia mitaani kwa siku ya tatu karibu na msikiti katika eneo la mji wa Cairo ambalo kwa kawaida ni ngome kuu ya chama chake, wakiimba kauli mbiu za hasira dhidi ya kile wanachokiita mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na jenerali wa jeshi Abdel-Fattah el-Sissi.

An Egyptian supporter of the Muslim Brotherhood walks holding a poster featuring deposed president Mohamed Morsi during a rally to support him on July 6, 2013 outside Cairo's Rabaa al-Adawiya mosque. Egypt's Islamists vowed further protests today to demand the army restore the country's first democratically elected leader, after a day of clashes which saw 26 people killed across the country. AFP PHOTO/MAHMUD HAMS (Photo credit should read MAHMUD HAMS/AFP/Getty Images)
Wapinzani wakiendelea na maandamanoPicha: Mahmud Hams/AFP/Getty Images

Jenerali huyo wa jeshi amekana kuwa amefanya mapinduzi ya jeshi, akisema kuwa alikuwa anachukua hatua za matakwa ya mamilioni ya Wamisri wanaoandamana dhidi ya rais huyo wa zamani.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / dpae

Mhariri: Amina Aboubakar