Manchester United na Manchester City | Michezo | DW | 16.04.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Manchester United na Manchester City

Bayern Munich ina miadi leo na Hannover 96

Nani (Kati) atamba baada ya bao lake

Nani (Kati) atamba baada ya bao lake

Mabingwa mara kadhaa wa Ujerumani,Bayern Munich wenye miadi na Olympique Lyon kwa nusu-finali ya Champions league baadae mwezi huu waitaka UEFA kufuta mpango wa kuahirisha mpambano wa mechi ya Ligi ya Lyon na Monaco. Kisa nini ?Bafana Bafana-Afrika Kusini yapiga kambi ya Ujerumani kujizoweza na hali ya hewa ya baridi itakayowakuta nyumbani Afrika Kusini wakati wa Kombe la dunia.Kinyan'ganyiro cha tikiti za Kombe hilo la dunia kilianza juzi na alao shabiki 1 alipoteza maisha huko Cape Town.

Bayern Munich, inadai isingependa jioni hii kuona mkosi uliowapata wenzao Schalke mwishoni mwa wiki iliopita walipozabwa mabao 4:2 na timu ya mkiani Hannover, ukawapata na wao.Katika Premier League Manu ina miadi na mahasimu wa mtaani Manchester City.Munich inacheza jioni hii na timu iliopo mkiani Hannover 96 lakini ndio ilioiasngusha Schalke Jumamosi iliopita.

Kocha wa Bayern Munich , van Gaal, ambayo ina miadi kwa mpambasno wa nusu-finali wa champions League na Olympique Lyon ya Ufaransa baadae mwezi huu, amelalamika kwa UEFA-shirikisho la dimba la ulaya na kulitaka ligeuze uamzi wa Ligi ya Ufaransa wa kuahirisha mpambano wa Ligi ya nyumbani kati ya Olympique Lyon na Munich.Munich inadai hatua hiyo inatoa nafuu isio haki kwa Lyon wakati munich inacheza mapambano yake ya Ligi ya nmyumbani.

Ligi ya Ufaransa, iliahirisha changamoto ya Lyon na Monaco, kufuatia ombi la Lyon .Lyon ilikuwa na changamoto na Monaco ili kutoana jasho hapo April24.Mpambano huo sasa umepangwa Mei 12.

Lyon lakini, imepangwa kucheza na Bayern Munich wiki ijayo April 21 na kwa duru ya pili April 27. Kwavile, Lyon mwishoni mwa wiki hii haina mchezo na ina muda wa kutosha wa kupumzika kabla ya duru ya pili na Munich, wenzao Munich ,wana kibarua kizito kuitimua nje Borussia Moenchengladbach hapo April 24. Munich, haitaki kuteleza, kwani, ina azma ya kutoroka na mataji yote 3 msimu huu:Kombe la champions league, Kombe la Taifa la Ujerumani na la Bundesliga. Munich, imewasili nusu-finali yake ya kwanza ya champions league, tangu ilipolitwaa kombe hilo mara ya mwisho 2001.

Tukigeukia Kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini, sio timu wenyeji Bafana Bafana, ililipiga kambi yake alao kwa siku 2 hapa Ujerumani, wiki hii ili kujizowesha na hali ya bnaridi itakayoikumba timu hiyo wakati wa kombe la dunia nyumbani hapo Juni, bali pia, firimbi ililia Afrika kusini, kuuza tiketi za Kombe hilo kama inavyofanyika kienyeji na sio kupitia mtandao ifanyavyo FIFA:

Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil, alipokutana na rais mwezake wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, hapo juzi huko Brazilia, alisema kwa mzaha wa kidiplomasia kuwa, anatumai finali ya Kombe la dunia 2010, itakua changamoto baina ya timu zao mbili:Brazil na Afrika Kusini.

"Ikiwa hujui , basi picha hii inaagua kuwa kukutana kwetu katika finali ya kombe la dunia 2010." Lula , aliwaambia waandishi habari pale marais hao 2 walipojumuika pamoja mbele ya wapigapicha.

Bafana Bafana, watafungua dimba Juni 11 na Mexico, wakiwa kundi A.Timu nyengine katika kundi hilo, ni Ufaransa na Uruguay.

Mabingwa mara 5 Brazil, watakaoandaa Kombe la dunia 2014 baada ya hili la Afrika, wako kundi G pamoja na Korea ya Kaskazini,Tembo wa Ivory Coast na Ureno. Wakati wa kinyan'ganyiro cha Kombe la mashirikisho-Confederations Cup mwaka jana,kinachotangulia Kombe la Dunia, Brazil iliipiga kumbo Afrika Kusini kwa bao 1-0 katika nusu-finali.

Kati ya wiki hii, watoto hao wa Bafana Bafana, walikuwa hapa Ujerumani kujizoweza na hali ya hewa ya baridi.Hii inafuatia mazowezi yao nchini Brazil ya kujiandaa kwa changamoto za Kombe la dunia 2010. Kocha wao mbrazil, Carlos Parreira,alijishughulisha zaidi kukiweka kikosi chake fit.Kilele cha maandalio ya Bafana Bafana, yatakayodumu hadi April 30,ni mpambano wao wa kirafiki na China hapo April 28, ingawa utachezwa wapi bado haijulikani.

Na huko Afrika Kusini, maalfu ya mashabiki wa dimba, walijipanga milolongo mirefu kununua tiketi za Kombe la dunia .Vituo 11 vya kuuzia tiketi vilifunguliwa katika miji yote 9 itayochezewa Kombe hilo. Mjini Cape Town, shabiki mmoja aliestaafu, alipinduka na kufariki dunia mapema alhamisi kabla kufunguliwa kituo akisubiri kujipatia tiketi yake. Tiketi ziko kwa mechi zote 64 kuanzia Juni 11 hadi finali Julai 11.

Mwandishi: Ramadhan Ali/rtr,afp.dpa

Mpitiaji:Abdul-Rahman,Mohammed