MANAGUA : Nicaragua kumchagua Rais mpya leo hii | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MANAGUA : Nicaragua kumchagua Rais mpya leo hii

Wapiga kura leo hii wanapiga kura nchini Nicaragua kumchagua Rais mpya wa nchi hiyo.

Kiongozi wa zamani wa wapiganaji wa chini kwa chini wa nchi hiyo Daniel Ortega inasemekana anaongoza katika uchaguzi huo. Akiwa anaungwa mkono na Urusi hapo zamani na kuchukiwa hadi leo hii na Marekani kiongozi huyo wa zamani wa Mapinduzi wa Nicaragua anataraji kurudi tena kwenye ngwe ya kisiasa kwa kujionyesha kuwa ni mtu mpenda amani, mtetezi wa demokrasia na mcha Mungu.

Serikali ya Marekani ina wasi wasi iwapo Ortega atashinda atashirikiana na Rais Hugo Chavez wa Venezuela kama sehemu ya kundi la kuipiga vita Marekani la viongozi wa Amerika ya Kusini.

Mpinzani mkuu wa Ortega ni mtaalamu wa benki wa zamani Eduardo Montealegre kutoka Muungano wa Kiliberali nchini humo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com