MANAGUA: Daniel Ortega aongoza katika uchaguzi wa urais nchini Nicaragua | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MANAGUA: Daniel Ortega aongoza katika uchaguzi wa urais nchini Nicaragua

Kiongozi wa zamani wa kikoministi nchini Nicaragua, Daniel Ortega, anaongoza kwa kura nyingi katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwishoni mwa wiki. Ameshapata asili mia 38 ya kura. Anahitaji asili mia 40 ya kura au asili mia 35 tu kukiwa na tofauti ya asili mia 5 ya kura kati ya yeye na mpinzani wake ili kuepuka duru ya pili ya uchaguzi. Mpinzani wake mkuu anayeungwa mkono na Marekani mwenye siasa za kihafidhina, Eduardo Montealegre, ameshapata asili mia 31. Wachunguzi wa Umoja wa Ulaya waliokwenda kusimamia uchaguzi huo, wamesema kwa jumla uchaguzi ulikwenda vizuri.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com