Man Utd yawawinda Schweinsteiger, Ramos | Michezo | DW | 10.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Man Utd yawawinda Schweinsteiger, Ramos

Vilabu vinaendelea na maandalizi ya kabla ya msimu mpya na kando ya timu kusafiri katika mataifa ya ng'ambo kwa ajili ya kambi za mazoezi ni wakati ambapo pia biashara ya usajili wa wachezaji imepamba moto.

Na mmoja wa wachezaji ambao wamekuwa wakimulikwa kwa muda mrefu ni nahodha wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger. Kwa mujibu wa Gazeti la Ujerumani la Bild, klabu ya Manchester United imetuma ombi la kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 wa klabu ya Bayern Munich kwa mkataba wa miaka miwili.

Inaripotiwa kuwa United inataka kumpa mshahara wa karibu euro million 10 kwa mwaka kiasi ambacho naibu nahodha huyo wa Bayern anapaka kwa sasa mjini Munich.

Kocha wa Man Utd Louis van Gaal amekuwa shabiki wa Schweinsteiger tangu mwaka wa 2009 – 2011 wakati alipoingoza klabu hiyo katika fainali ya Champions League ya mwaka wa 2010. Van Gaal pia anaripotiwa kumwinda mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Sergio Ramos kutoka Rea Madrid.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman