Man United yalazwa na Liverpool, Juventus yashinda | Michezo | DW | 30.07.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Man United yalazwa na Liverpool, Juventus yashinda

Juventus walikuwa wanacheza na Benfica huko New Jersey Marekani katika mechi ya matayarisho ya msimu mpya na wakatoka sare ya bao moja kwa moja

Juventus lakini wakasonga mbele na kushinda mechi hiyo 4-2 baada ya kupiga mikwaju ya penalti. Manchester United wao walikuwa wanacheza na Liverpool na wakapokea kipigo cha 4-1. Sadio Mane aliwafungia Liverpool goli la kwanza kisha Andreas Perreira akasawazisha kabla Daniel Sturridge, Sheyi Ojo na Xherdan Shaqiri hawajawafungia Liverpool magoli yao kwenye kipindi cha pili.

Kuhusu Manchester United, kocha wao Jose Mourinho amewataka wachezaji wake walioshiriki Kombe la Dunia kuupunguza muda wao wa likizo ili waisaidie timu yao katika mechi za ufunguzi kwenye ligi kuu ya England. Wachezaji kadhaa wa United wakiwemo Paul Pogba, Romelu Lukaku na Jesse Lingard wako mapumzikoni na huenda wakakosa kushiriki mechi ya kwanza ya klabu hiyo dhidi ya Leicester City tarehe 11 Agosti, hiyo ikiwa chini ya wiki mbili.

"Ninafurahia mechi, jinsi uchezaji unavyobadilika, lakini sina wachezaji wa kufanya kazi nao. Sina idadi kubwa ya wachezaji watakaokuwa kwenye kikosi tarehe 9 Agosti pale soko la uhamisho wa wachezaji, kwa hiyo sifurahii kuwa na wachezaji wachache," alisema Mourinho.

Kulingana na Mourinho Phil Jones na Marcus Rashford watafupisha likizo zao.

Mwandishi: Jacob Safari

Mhariri: Yusuf Saumu