Malawi inakabiliwa na uhaba wa madaktari | Matukio ya Afrika | DW | 29.04.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Malawi inakabiliwa na uhaba wa madaktari

Sekta ya afya nchini Malawi inatajwa kuwa miongoni mwa sekta zinazokabiliwa na changamoto kubwa kutokana na upungufu wa madawa, madaktari wa kawaida na madaktari bingwa.

Rais wa Malawi Malawi Joyce Banda

Rais wa Malawi Malawi Joyce Banda

Akizungumza na shirika la habari la IPS, Dokta Theresa Allain, profesa na mkuu wa kitengo cha afya katika chuo kikuu cha kimataifa cha afya mjini Blantyre, amesema sekta ya afya nchini Malawi imedorora kutoka na kasumba ya madakatari bingwa na wauguzi kwenda nje kufanya kazi katika nchi ambazo wanadai zinalipa mishahara mizuri kwa wataalamu hao.

Anasema hali hiyo imesababisha maradhi mengi kutofanyiwa vipimo sahihi kutokana na wauguzi wengi kutokuwa na uelewa mkubwa wa kujua vyanzo mbalimbali za maradhi na vipimo vinavyotakiwa kutumika kupima maradhi hayo.

Kwa mujibu wa Dk.Allain,tatizo hilo linatakiwa kuangaliwa kwa upana zaidi na sio upande mmoja na kwamba kuna haja ya kupata wataalamu wenye ujuzi mkubwa wa kitabibu, licha ya kuwa hakuna waganga wa kutosha kushika nafasi hizo.

Mbali na hilo profesa Allain amesema kuwa licha ya wizara ya afya ya nchi humo kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya mafunzo kwa madakatari hao lakini bado huduma za afya na dawa katika hospitali mbalimbali nchini humo ni tatizo kubwa

Profesa Allain amesema kuwa kwa sasa Malawi ina mpango wa kutoa mafunzo kwa kwa madakatari wa magonjwa maalumu kwani kwa sasa taasisi yake ya elimu imekomaa kutoa huduma hiyo ya maendelo.

''Tunahitaji waganga wa maradhi malumu ambao watakuwa na ujuzi wa hali ya juu ambao utawawezesha kutibu magonjwa sugu ndani ya nchi'', ameongeza Profesa Allain akiongeza kuwa ujuzi huo utasaidia kutibu magonjwa ya moyo, kiharusi, presha na maradhi ya ukimwi.

Andrew Mataya, mwenye umri miaka 28, mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika chuo cha afya nchini Malawi anasema kuwa anahitaji kusomea fani maalumu lakini inakuwa ngumu kuchukua maamuzi, kwani inategemea na asili ya fani hiyo na uhusiano wake na wasimamizi wa vitengo hivyo, na mahitaji ya serikali kwa sasa.

Uchache wa Madaktari bado ni tatzo

Mwananchi wa Malawi

Mwananchi wa Malawi

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani DHO ya mwaka 2010 imegundua kuwa Malawi ina Madakatari 257 ambao wanahudumia watu zaidi ya Milioni 15 na kwa sasa kuna wakufunzi ambao 459 ambao tayari wamesajaliwa na baraza la Afya la Malawi.

Mbali na kuongezeka idadi ya watu hao nchini malawi lakini bado kuna madaktari bingwa 177 nchi nzima na kuna upungufu m kubwa wa Madakatari,ambapo Dokata mmoja anatibia 33,300

Hali hiyo pia inapatikana nchini Kenya ambapo jumla ya Madakatari Bingwa 1,654 waliosajaliwa na inakadiriwa kuwa Dokta mmoja anatibia wagonjwa 5,190, wakati Kusini ya Malawwi na Afrika Kusini jumla ya madaktari bingwa 9,600 ambapo kila dakatari mmoja anatibia wagonjwa1,320.

Kwa sasa Malawi imekuwa ikifanya juhudi za kupambana upungufu wa rasimali watu katika sekta ya afya kama wauguzi ambao wanatakiwa kufanya kazi za kupiga sindano,kufanya vipimo vya HIV na shuguli zingine za kiafya.

Licha ya kuwa Malawi imekuja na mpango wa kusomesha zaidi madakatari ndani ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa madakatari katika hospitali nchini humo,lakini mpango huo unatajwa kuwa matunda yake huenda yakachukua muda mrefu, kupata madakatari bingwa watakahudumia hospitali kuu za mjini na wilayani.

Mwandishi: Hashim Gulana /IPS

Mhariri: Mohammed Khelef