1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makundi ya kibinaadamu Somalia yatangaza ukame nchini humo

Lilian Mtono
26 Aprili 2021

Makundi ya misaada ya kibinaadamu jana yametangaza hali ya ukame nchini Somalia, yakionya kwamba mamilioni wanakabiliwa na njaa katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.

https://p.dw.com/p/3saRk
Ausnahmezustand in Somalia
Picha: picture-alliance/AP/B. Curtis

Taarifa ya pamoja ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia pamoja na wizara ya masuala ya maafa na majanga imesema kwamba zaidi ya asilimia 80 ya taifa hilo inakabiliwa na ama ukame wa wastani ama mbaya kabisa.

Mvua za chini ya kiwango kwa zaidi ya miezi miwili huenda zikachochea mazingira ya ukame kuwa mabaya zaidi katika eneo kubwa la nchi hiyo.

soma  zaidi:Amnesty International: Wakimbizi wa ndani nchini Somalia wakabiliwa na dhiki kubwa

Mashirika hayo ya kibinaadamu kwa pamoja yamesema yatahitaji dola bilioni 9 ili kuwasaidia watu milioni 4 wenye mahitaji.

Azimio hilo linatolewa wakati Somalia ikiwa inakabiliwa na janga la virusi vya corona, mzozo wa kisiasa na mashambulizi ya mara kwa mara ya kigaidi.