1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano yatiwa saini Yemen

22 Mei 2011

Waakilishi wa upinzani nchini Yemen, wametia saini makubaliano yaliyopendekezwa na nchi za Ghuba, yakimtaka Rais Ali Abdallah Saleh kuondoka madarakani katika kipindi cha siku 30 na badala yake hatofikishwa mahakamani.

https://p.dw.com/p/RPKp
Yemeni President Ali Abdullah Saleh speaks during a media conference in Sanaa, Yemen, Monday, Feb. 21, 2011. Yemen's president rejected demands that he step down and said Monday that the widespread demonstrations against his regime were unacceptable acts of provocation, though he renewed calls for talks with the protesters. After a week and a half of marches that have left nine dead, President Ali Abdullah Saleh told a news conference that he ordered the army to fire at demonstrators "only in case of self-defense." (Foto:Hani Mohammed/AP/dapd)
Rais Ali Abdullah Saleh wa YemenPicha: dapd

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema, wajumbe watano wa upinzani wametia saini makubaliano hayo mbele ya mabalozi wa kigeni. Kwa mujibu wa upinzani, miongoni mwa wageni hao ni wajumbe wa Marekani, Umoja wa Ulaya na Baraza la Ushirikiano wa Kiuchumi la Nchi za Ghuba.

Hii leo, Rais Saleh anatazamiwa kuidhinisha makubaliano hayo. Serikali ya umoja wa kitaifa itakayoongozwa na upinzani, inapaswa kuundwa katika kipindi cha wiki moja.Yemen imekumbwa na machafuko na maandamano dhidi ya Saleh, anaetawala kwa takriban miaka 33 nchini humo.

Jemen, Sanaa, Yemen, Demonstrationen gegen Staatspräsidenten Ali Abdullah Saleh. Rechte: DW- Korrespondent im Jemen Saeid Al-Soffi 13.5.2011
Maandamano dhidi ya Rais Ali Abdulla SalehPicha: DW