Makubaliano ya Nord Stream 2 yazua hofu ya uchokozi wa Urusi mashariki mwa Ulaya | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.07.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Makubaliano ya Nord Stream 2 yazua hofu ya uchokozi wa Urusi mashariki mwa Ulaya

Ukraine na Poland zakosoa makubaliano ya Marekani na Ujeruamni ya kuruhusu kukamilika kwa bomba la kubeba gesi ya Urusi, zikisema kuwa ni tishio kubwa la usalama na jeshi mashariki mwa Ulaya.

Kwa nchi nyingi za Ulaya ya kati na mashariki, bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Urusi kwenda Ujerumani liitwalo Nord Stream 2 haliangaliwi tu kama ni mradi wenye utata mkubwa. Bali pia, wanauangalia kama kipimo cha uaminifu wa Ujerumani katika eneo hilo. Na, hivi sasa, uaminifu huo uko katika hali mbaya.

Makubaliano ya wiki hii kati ya Marekani na Ujerumani kuhusu mgogoro huo wa Bomba la Gesi la Nord Stream 2, yameafiki kuwa mradi huo utakamilishwa bila ya Marekani kuuwekea vikwazo zaidi. Uamuzi huo umezua hasira na hofu miongoni mwa mataifa mengi ya mashariki mwa Ulaya yanayouangalia mradi huo kama tishio la usalama wao.

Soma zaidi: Marekani na Ujerumani zafikia muafaka mradi wa bomba la gesi la Urusi

Kwa nchi kama Ukraine, Poland na haswa mataifa ya Baltiki, lakini pia Rumania suali ni je, ukosoaji wa Ujerumani wa ya sera ya kigeni ya kichokozi ya Rais Vladimir Putin ni wa kweli, au Ujerumani itaweka mbele zaidi maslahi yake ya kiuchumi badala ya kushikilia msimamo wake wa kuikosoa Urusi.

Ukraine, Poland wakosoa makubaliano ya Ujerumani na Marekani

Ukraine, ambayo imekuwa ikipingana na Urusi tangu ilipoinyakua rasi ya Crimea mwaka 2014, na Poland wamekosoa vikali makubaliano ya Ujerumani na Marekani, ambayo yanasafisha njia ya bomba hilo kuanza kufanya kazi.

USA I Angela Merkel und Joe Biden in Washington

Angela Merkel na Joe Biden wakiwa Ikulu ya Mreakni, Washington

Tamko la pamoja la mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yote mawili, Dmytro Kuleba na Zbigniew Rau, limesema kwamba "uamuzi wa kusita kupinga ujenzi wa bomba hilo la Nord Stream 2 utasababisha kuwepo tishio la kisiasa, kijeshi na kinishati kwa Ukraine na Ulaya ya kati, huku Urusi ikiimarisha uwezo wake wa kudhoofisha hali ya usalama barani Ulaya."

Andriy Yermak, mkuu wa ofisi ya Rais wa Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy, amesema bomba la gesi la Nord Stream 2 ni kama sialaha ambayo Urusi hakika itaitumia dhidi ya Ukraine na bara zima la Ulaya.

Ukraine yahofia tishio kubwa la usalama

Kateryna Odarchenko, mchambuzi wa kisiasa na mkurugenzi wa Tasisi ya Demokrasia ya PolitA na Maendeleo mjini Kyiv, Ukraine, amesmea kwamba bomba la Nord Stream 2 ni tishio kwa Ukraine - na sio tu kwa sababu nchi hiyo itapoteza mabilioni ya euro ya malipo iliokuwa ikiyapata kusafirisha gesi ya Urusi hadi barani Ulaya.

Deutschland | ukrainischer Präsident Wolodymyr Selenskyj in Berlin

Angela Merkel na Volodymyr Zelensky mjini Berlin, July 12, 2021

Ameiambia DW kwamba mara tu Urusi itakapokuwa haitumii tena mabomba ya Ukraine kusafirishia gesi yake, basi itayaharibu na hilo linaamisha kitisho cha kuzuka vita Ukraine kitaongezeka.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Naftogaz ya Ukraine, Yuriy Vitrenko, amesema haamini ahadi za Ujerumani za kunahakikisha kuwa usafirishaji wa gesi ya Urusi kupitia Ukraine utaruhusiwa kuendelea

"Gesi ya Urusi itakapokuwa haipiti tena Ukraine, basi na matukio ya uchokozi ya jeshi la Urusi yataongezeka pakubwa," Vitrenko aliiambia Idhaa ya Ukraine ya VOA katika matamshi yaliyotafsiriwa kwenye tovuti yao.

Sikiliza sauti 09:45

Ujenzi wa bomba la Nord Stream 2 uko njia panda.

Poland pia inahofia uchokozi wa Urusi

Makubaliano ya kati ya Ujerumani na Marekani pia yalikosolewa nchini Poland wiki hii. "Tumesisitiza tangu mwanzo kabisa kwamba mradi wa kijiografia wa Nord Stream 2 utatibua utulivu wa hali ya kisiasa katikati na mashariki mwa Ulaya," msemaji wa serikali Piotr Mueller aliwaambia waandishi wa habari, na kuongeza kuwa "Poland haikubaliani na hilo."

Mueller amesema serikali ya Poland "ilishangazwa" na makubaliano ya Ujerumani na Marekani na kwamba Ujerumani "kwa bahati mbaya inaungwa mkono masilahi ya Urusi," amesema Mueller. Aliongeza kuwa, kwa bahati mbaya, hakukuwa na jibu la kuridhisha kutoka Umoja wa Ulaya.

Russland | Deutschland | Handschlag Merkel und Putin

Angela Merkel akipeana mkono na Vladimir Putin

Mtaalam wa Nishati Robert Tomaszewski wa Taasisi ya Polityka Insight yenye makao yake mjini Warsaw ameiambia DW kwamba msimamo wa Poland huenda ukawa sawa na ule wa Ukraine kwenye suala la bomba la gesi la Nord Stream 2. Wakati huo huo, amesema, uhusiano na Marekani na Ujerumani huenda ukapowa zaidi.

Amesema kumekuwa na hofu nchini Poland kwamba Marekani kuridhia ujenzi wa bomba hilo, kutaipa fursa Urusi kuzidisha vitendo vya uchokozi dhidi ya Ukraine na eneo lote la kati na mashariki mwa Ulaya.