1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya kuweka chini silaha Hodeida nchini Yemen

Oumilkheir Hamidou
14 Desemba 2018

Umoja wa Mataifa umefanikiwa kuzishawishi pande zinazohasimiana nchini Yemen ziweke chini silaha katika mji muhimu wa bandari wa Hodeida

https://p.dw.com/p/3A5wx
Schweden | Friedensgespräche Jemen-Konflikt in Rimbo
Picha: picture-alliance/dpa/TT NYHETSBYRÅN/P. Lunahl

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na mjumbe wake maalum Martin Griffiths wanasaka ufumbuzi wa kudumu baada ya miaka minne ya vita vilivyoangamiza maisha ya watu wasiopungua 10.000 na kutishia  hadi watu milioni 20 kufa kwa njaa.

Wapatanishi ambao hawakuwa na matumaini makubwa ya kupatikana maridhiano, wamesema pande hizo mbili zimepangiwa kukutana tena  mwishoni mwa mwezi january mwakani ili kujaribu kufafanua mwongozo wa majadiliano yatakayosaidia kupatikana ufumbuzi wa kisiasa.

"Hadi wakati huo, makubaliano ya Rimbo yatasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya wananchi wa Yemen" amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

KIkao cha baraza la Ualama la Umoja wa Mataifa mjini New-York
KIkao cha baraza la Ualama la Umoja wa Mataifa mjini New-YorkPicha: picture-alliance/dpa/S. Wenig

Baraza la usalama kuidhinisha kutumwa wasimamizi Hodeida

Baraza la Usalama la umoja wa mataifa litaarifiwa leo mjini New-York , matokeo ya mazungumzo ya Rimbo, kijiji cha karibu na Stockholm nchini Sweeden. Baraza la usalama la Umoja wa mataifa linatazamiwa kupitisha azimio wiki inayokuja  kuidhinisha makubaliano hayo na kuruhusu wasimamizi wasiopungua 30 wapelekwe katika eneo hilo.

Makubaliano ya kuweka chini silaha yataanza hivi karibuni mjini Hodeida, mji wa bandari unaopakana na bahari ya Sham zinakotia nanga meli  nyingi zinazoingiza misaada nchini humo ambakpo, kwa mujibu wa umoja wa mataifa ndiko linakopiga balaa kubwa kabisa kuwahi kuwathiri binaadam.

Vikosi vya serikali inayosadiwa na ushirika wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia na wapiganaji wa hotuhi wanaosaidiwa na Iran watabidi wauhame mji huo pamoja na bandari yake.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa marekani Mike Pompeo akihutubia baraza la Usalama la umoja wa mataifa
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa marekani Mike Pompeo akihutubia baraza la Usalama la umoja wa mataifaPicha: picture-alliance/AP/M. Altaffer

Baraza la Seneti la Marekani laihimiza Marekani isitishe misaada ya kijeshi kwa Saudi Arabia

"Umoja wa Mataifa utakuwa na jukumu muhimu" amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Jumuia ya kimataifa imesifu makubaliano yaliyofikliwa. Hata hivyo baadhi ya mashirika ya misaada ya kiutu yanayataja makubaliano hayo kuwa ni "hatua ndogo tu". Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani MIke Pompeo ameyataja makubaliano hayo kuwa "hatua muhimu na kwamba amani inawazekana."

Nchini Marekani kwenyewe  baraza la Seneti limepitisha azimio linalopiga marufuku aina yoyote ya msaada wa kijeshi kwa Saudi Arabia katika vita nchini Yemen.

 

 

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AFP/dpa/SP

Mhariri: Mohammed Khelef