1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya Copenhagen

20 Desemba 2009

Kansela Angela Merkel asema uamuzi Copenhagen ulikuwa mgumu kwake binafsi.

https://p.dw.com/p/L97y
Wanaharakati wa mazingira waukosoa mktaba wa Copenhagen.Picha: AP

Baada ya siku 13 za jitihada za kupata mkataba wa makubaliano, mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa umemalizika mjini Copenhagen. Wajumbe walikiri kwamba makubaliano yaliyoafikiwa jana, hayakutimiza malengo yaliyokuwa yamewekwa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliutaja mkataba huo wa Copenhagen kama hatua muhimu, lakini akasema bado kuna kazi kubwa.

Kwa mara ya kwanza kabisa, mkataba huo wa Copenhagen uliweka viwango vya kupunguza gesi inayoharibu mazingira  kuwa nyuzi joto mbili na kuahidi kitita cha dola bilioni 100 kuyasaidia mataifa maskini kupambana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mkutano huo ulioyaleta pamoja mataifa 193 katika mji mkuu wa Denmark Copenhagen ulimalizika na mkataba ambao hauwajibiki kisheria uliokubaliwa na viongozi wa Marekani, China India, Brazil na Afrika Kusini. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alielezea kutoridhishwa kwake na udhaifu wa mkataba huo, akisema uamuzi huo ulikuwa mgumu sana kwake binafsi.