1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya amani ya Sudan

Oumilkher Hamidou20 Agosti 2009

Pande zinazoshindana zimekubaliana kuzungumzia vifungu vinavyobishwa vya makubaliano ya amani ya mwaka 2005

https://p.dw.com/p/JEdx
Vikosi vya Umoja wa mataifa vyalinda amani kusini mwa SudanPicha: DW

Maafisa wa kisiasa wa ngazi ya juu kutoka kaskazini na kusini mwa Sudan wameahidi hapo jana kuvishughulikia vifungu vinavyobishwa vya makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2005.Ahadi hiyo inatokana na juhudi za upatanishi za mjumbe maalum wa Marekani Scott Gration.

Scott Gration amesema makubaliano hayo mepya ni matokeo ya miezi kadhaa ya majadiliano kuhusu vifungu vinavyozusha mabishano vya makubaliano ya amani,ikiwa ni pamoja na mpango ambao hadi sasa bado haukutekelezwa wa kuchora mpaka wa maeneo ya kaskazini na yale ya kusini na masuala yanayohusu usalama.

""Mpango wa kivitendo" umelengwa kuyapa msukumo" makubaliano jumla ya amani-yaliyotiwa saini mwaka 2005 na chama cha National Congress-NCP- cha rais Omar el Bashir na waasi wa zamani wa kusini wa kutoka chama cha SPLM" nchini Kenya.

Vyama hivi viwili ambavyo uhusiano wao ungali bado ni tete,vimekubaliana kuzipatia pia ufumbuzi mada tete mfano wa uchaguzi mkuu uliopangwa kuitishwa mwezi April mwakani,,jinsi ya kugawana madaraka na pia juhudi za amani katika jimbo la magharibi la Darfour.

"Makubaliana haya yatarahisisha ushirikiano na kuimarisha uhusiano ambao,nnaamini,utaleta tija katika mustakbal wa Sudan" amesema mjumbe huyo wa Marekani,Scott Gration,wakati wa sherehe za kutia saini makubaliano hayo huko Juba-mji mkuu wa eneo la kusini la Sudan.

"Tumetaka kwa namna fulani kushadidia nia yetu na kupanga lini tunafikiria kuendeleza majadiliano ziada."Amefafanua mshauri wa rais Omar el Bashir-Ghazi

Salehedine.

Vipengee viwili vimetengwa na mpango huo wa kivitendo:navyo ni kuhusu vielelezo vya kura ya maoni ya uhuru wa eneo la kusini mwa Sudan iliyopangwa kuitishwa mwaka 2011 na matokeo ya kuhesabiwa idadi ya wananchi jumla wa Sudan ambayo yatahitajika kwaajili ya kugawa vituo vya upigaji kura kwa uchaguzi wa mwezi April mwakani.

Brüchiger Frieden im Südsudan - Warnung vor Landminen
Onyo-miripuko imezikwa ardhini kusini mwa SudanPicha: DW

Vipengee hivyo vitajadiliwa duru nyengine ya mazungumzo itakapoitishwa mwezi September mwaka huu kati ya wawakilishi wa NCP,SPLM na mjumbe huyo maalum wa Marekani Scott Gration.

Leo hii Scott Gration amepanga kwenda Malakal,mji muhimu wa eneo la kusini la Sudan ambako mapigano kati ya makundi ya waasi wa kaskazini na wale wa kusini yamegharimu maisha ya ya watu kama 50 hivi mapema mwaka huu.

Jana pia watu watatu wameuwawa kufuatia mapigano ya ya kikabila katika jimbo tajiri kwa mafuta kusini mwa Sudan.

Mwandishi Hamidou Oummilkheir(AFP/Reuters)

Mhariri M.Abdul Rahman