MAKASSAR: Ndege ya abiria yaendelea kutafutwa | Habari za Ulimwengu | DW | 03.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MAKASSAR: Ndege ya abiria yaendelea kutafutwa

Waokoaji wameanza tena leo kuitafuta ndege ya abiria katika eneo la mashariki mwa Indonesia ambayo mpaka sasa haijulikana iliko.

Jana maofisa wa Indonesia walitangaza kimakosa walikuwa wameipata ndege hiyo aina ya Boeing 737 katika eneo la milimani na kwamba abiria 12 walikuwa wamenusurika na wengine 90 walikuwa wamekufa.

Afisa anayeongoza juhudi za kuitafuta ndege hiyo, Bambang Karnoyudho, amesema meli tatu za jeshi la wanamaji na ndege tano za jeshi la angani zimetumwa katika maeneo ya magharibi mwa Sulawesi na upande wa baharini.

Inahofiwa mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo huenda ikawa kikwazo kikubwa na kutatiza juhudi za uokozi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com