1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGhana

Makamu wa Rais wa Marekani awasili nchini Ghana

26 Machi 2023

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, amewasili hii leo mjini Accra nchini Ghana ambako amesema ana matumaini na mustakabali wa Afrika.

https://p.dw.com/p/4PGYm
Ghana | US Vize Präsidentin Kamala Harris in Accra
Picha: NIPAH DENNIS/AFP/Getty Images

Kamala Harris anatarajiwa hiyo kesho kukutana kwa mazungumzo na rais wa Ghana Nana Akufo-Addo.

Harris anaanza ziara yake ya wiki moja barani Afrika katika juhudi za kuboresha uhusiano kati ya nchi yake na bara hilo lakini pia kukabiliana na ushawishi wa China unaoongezeka barani humo.

Akiambatana na muwewe Doug Emhoff, Kamala Harris atazitembelea pia Tanzania na Zambia, huku akiangazia zaidi maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na ongezeko la idadi ya vijana. Rais Joe Biden anatarajiwa pia kufanya ziara barani Afrika baadaye mwaka huu.