Majumba yachomwa moto London; ghasia zaendelea | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.08.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Majumba yachomwa moto London; ghasia zaendelea

Moto umeendelea kuwaka mjini London kwa siku ya tatu mfululizo wakati ghasia na hali isiyo tulivu vikiongezeka. Waziri mkuu David Cameron amekatiza mapumziko yake nchini Italia.

default

ePolisi wa Uingereza wakiwa wamesimama karibu na jengo lililochomwa moto mashariki ya London

Moto unaendelea kuwaka mjini London kwa siku ya tatu mfululizo wakati ghasia na hali isiyo tulivu vikiongezeka. Waziri mkuu David Cameron amekatisha mapumziko yake nchini Italia na kurejea mjini humo na anatarajiwa kukutana na kamati ya ngazi ya juu ya kushughulikia masuala ya dharura leo Jumanne. Wakati huo huo , ghasia hizo , ikiwa ni pamoja na uporaji ,uchomaji magari na majengo , umesambaa katika maeneo mapya mjini London na katika miji ya Birmingham na Liverpool. Ghasia hizo zilianzia Tottenham siku ya Jumamosi baada ya maandamano dhidi ya polisi kugeuka kuwa ghasia. Hata hivyo waziri wa mambo ya ndani Theresa May ameshutumu ghasia hizo kuwa ni uhalifu.

Großbritannien Abhörskandal David Cameron in Wales

Waziri mkuu David Cameron amekatiza mapumziko yake nchini Italia na kurejea mjini London.

 • Tarehe 09.08.2011
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12DFi
 • Tarehe 09.08.2011
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12DFi
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com