1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majina ya wapigaji kura yabandikwa vituo vya kupigia kura Tanzania

25 Oktoba 2010

Hali ni shwari katika kisiwa cha Pemba

https://p.dw.com/p/PnjR
Watanzania wakisubiri kwa hamu uchaguzi wa Oktoba 31 mwaka huuPicha: Mohammed Khelef

Huko nchini Tanzania, wakati ambapo ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, tume mbili za uchaguzi ile ya taifa inayosimamia uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar, zimetoa majina ya wapiga kura ambayo yamebandikwa katika vituo vya kupigia kura.

Katika kisiwa cha Pemba, kufuatia muafaka uliofikiwa kati ya chama tawala CCM, na kile cha upinzani, CUF, safari hii mpaka muda huu hakuna malalamiko yoyote kuhusiana na majina hayo, tofauti na chaguzi zilizopita. Hayo na mengine alinifahamisha mwandishi wetu wa huko Zanzibar, Salma Said, ambaye kwa sasa yuko Pemba.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Othman Miradji