MAJESHI YA MAREKANI IRAQ | Habari za Ulimwengu | DW | 24.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MAJESHI YA MAREKANI IRAQ

WASHINGTON:

Baraza la waakilishi nchini Marekani limepiga kura na kuweka muda wa mwisho kuwa August 31,mwakani kwa majeshi ya Marekani kuihama Iraq.Baraza hilo la waakilishi ambamo wademocrat wana wingi lilipitisha azimio hilo kwa kura 218 dhidi ya 212.

Hii inaangaliwa kuwa changamoto kubwa kabisa hadi sasa kwa rais George Bush .Kura katika baraza hilo imefuata misingi ya utiifu wa chama.Warepublican wameonesha wameungana pamoja kulipinga azimio hilo.

Rais Bush baadae aliwaambia maripota kwamba hatatia saini kuligeuza azimio hilo kuwa sheria.Wiki ijayo, Baraza la senate latazamiwa pia kulipigia kura azimio hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com